Blogger Widgets

October 18, 2013

Ujumbe wa Masister Duu wanaovaa Nguo Fupi Kama Hivi


Habari zenu

Leo niko na nyie dada zangu ninaowaheshimu na kuwapa heshima mnayostahili!!


Back to the topic,.


Ninakereka sana na vijivazi vyenu mnavyovivaa siku hizi kwa kuwa haviendani kabisa na utamaduni wetu wa kitanzania na unapoteza maadili kabisa katika jamii husika, siyo wakina dada wala akina mama, wote wamejisahau kabisa, unamkuta mdada/mama amekuvalia mini-skirt kiasi kwamba nusu kama siyo robo tatu ya maumbile yake anayaacha wazi,.


Sijui mnafanya makusudi ama vipi maana bado sijapata jibu mpaka sasa, wengine wanasema mnawatega wanaume ili waingie kingi, wengine wanasema ndiyo kuendana na wakati hivyo yaani ni taabu tupu dada zangu, kwanini msivivae hivi vijivazi mkiwa na mabwana zenu humo vyumbani kwenu muwaonyeshe neema mlizojaaliwa ili wawafurahie maana ndiyo wanaostahili kuyaona maumbile yenu?.Badilikeni ili jamii iwarejeshee heshima yenu tafadhali!!!