Blogger Widgets

October 8, 2013

Umeisikia Hii ya Redsan wa Kenya na Brick & Lace wa Jamaica?

Tumeshashuhudia collabo nyingi za wasanii wa Afrika Mashariki na wasanii wa kimataifa, tukianzia hapa kwetu collabo ya hivi karibuni ya Ommy Dimpoz na J. Martins wa Nigeria ambayo ni hit song kwa sasa ‘Tupogo’, AY na Sean Kingston ambayo bado haijatoka, na hit Song ya Wyre na Alaine wa Jamaica ‘Nakupenda pia’.
Redsan
Tutegemee collabo nyingine ya kimataifa kati ya star wa dancehall Kenya Redsan na mmoja kati ya ndugu wawili Brick & Lace wa Jamaica waliowahi kuhit na single yao iitwayo ‘Love is wicked’.
Brick and Lace

Kwa mujibu wa Gheto radio ya Kenya Redsan yuko katika mazungumzo na ndugu hao Nyanda na Nalia Thourborne aka Brick n lace lakini bado haijakuwa wazi ni yupi kati yao atakayehusika na collabo hiyo.
Hit maker wa ‘Badder Than Most’ iliyotengenezwa na producer mtanzania Sappy katika studio za Homeboys, Redsan ni miongoni mwa wasanii wa Afrika mashariki ambao wamesaini mkataba na label ya kimataifa ya Rockstar 4000 hivi karibuni.