Blogger Widgets

November 23, 2013

Audio:B'Hits yatoa ufafanuzi kuhusu kuwaondoa Mabeste, Vanessa na Gosby, na maelezo anayotoa Mabeste.Je watalipa damages za mkataba?








Jana (November 21) B’Hitz Music Group iliweka wazi uamuzi wa kuwaondoa kwenye label hiyo wasanii watatu ambao ni Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby.


Japokuwa Vanessa na Mabeste walitangaza wiki hii kujitoa kwenye label hiyo, huku Gosby akiwa bado hajasema chochote, timu ya BHits imesema kuwa wasanii hao waliondolewa kwenye label hiyo miezi miwili iliyopita japokuwa hawaamua kutangaza.


Mabeste aliiambia Times fm kuwa ameamua kujiondoa katika label hiyo kwa kuwa muziki wake ulikuwa haumlipi na kwamba maisha aliyokuwa anaishi ndiyo yaliyopelekea yeye kudhaniwa kuwa anafanya show za nje, na kwamba amechoka kuwa mzigo kwao.


Tovuti ya Times fm ilimtafuta Amani Joachim ambaye ni mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits Music Group ili kufahamu kuhusu sababu alizozitoa Mabeste kwa upande wa B’Hits, na mikataba ikoje na kama watachukua hatua zozote za kisheria.


“Hiyo statement ambayo Mabeste ameamua kuisema kwangu mimi naona haiko sawa kabisa. Sisi ni ndugu na tulikuwa tunaishi hivyo, tatizo la mtu mmoja ni tatizo la mtu mwingine yaani tunakuwa pamoja kabisa. Na kuna vitu vingi ambavyo Mabeste anajua kwamba tunavifumbia macho. Hata hiyo mikataba, sisi na Mabeste kuna kipindi tume-deal hata bila mikataba na mambo yakawa safi tu kwa sababu kuna ile heshima na kuaminiana.” Amesema Amani.


Ameyaelezea pia madai ya Mabeste kuwa mabadiliko yake katika maisha ndiyo yaliyosababisha B’Hits kuhisi kwamba anapiga shows za nje.


“Mabeste inabidi aangalie statements zake, na muda ambao anaamua kutoa hizo kauli kwa sababu kati yetu sisi tuna siri nyingi sana (Mabeste na Upande wa B’Hits). Tusifike sehemu kwamba tukaanza kufaidisha kila mtu, hicho ndicho kitu ambacho ningependa kukiweka sawa. Hizo shows na vitu vingine ambavyo labda alikuwa anavifanya akiwa nje tunavifahamu vingi tu, lakini kutokana na ule u-brother na nini tunavichunia tu.” Ameeleza kiongozi huyo wa B Hits.


Hata hivyo Amani amekubaliana na kuwepo kwa ubovu wa soko la muziki ambapo amesema hata shows zikiwepo bado malipo yanayotolewa yako chini kiasi kwamba Kampuni haliwezi kuendeshwa kwa kutegemea kugawana kipato hicho na msanii.


Aliongelea pia madai ya Mabeste kuwa B’Hits haikuwa inamfanya atengeneze pesa kupitia muziki wake.


“Well, hopefully kule anakoenda atapata. Tunaelewa Mabeste ana majukumu, maisha yake tunajua kwamba yamebadilika kwa namna flani. Personally nafahamu, sijui akina Harmy na Pancho. That’s why I’m ready to stay quiet kwenye vitu kama hivyo, nilikuwa tayari kukaa kimya…sina haja ya kufunguka ni vitu vingapi ambavyo Mabeste ameshafanyiwa katika hali ya u-brother, I will not say them kwa sababu kipindi mimi navifanya nilivifanya katika good will na nilitaka iishie hivyo, Amani will never say them.”


C.E.O wa B'Hits Hermy B aliuambia mtandao wa Bongo5 kuwa Vanessa, Gosby na Mabeste hawana shukurani kwa kile ambacho B Hits imewafanyia na kutoa mfano kuwa alitoa shilingi million nane mfukoni kulipia video ya Closer ya Vanessa  na kiasi kingine kulipia kazi alizofanya nje ya studio za B Hits, fedha ambazo hazijawahi kurudi.


Nae Amani Joachim alitoa ushauri kwa Vanessa, Mabeste na Gosby kwa ujumla kuwa wawe na amani na waendelee kufanya mambo yao na kuacha kutengeneza vita kati yao na B’Hits kupitia media kwa kuwa hata yeye ameamua kuyafumbia macho mengi.  


Lakini vipi kuhusu hasara ambayo B’Hits itaipata kutokana na kuondoka kwa wasanii hao kwa kuwa walichukuliwa wakiwa hawana majina na wakati huu wanaondoka wakati wameanza kuwa productive.


Mwana sheria na Chief Operations Officer wa B’Hits
anaeleza.


“They were real productive na naweza kukwambia kweli hawa watu wako very talented, na B’Hits haijawahi kum-house mtu ambaye ni mbovu, na ndo maana watu wanashangaa kwa nini mna nyumba kubwa ya media halafu mna watu watatu tu, sisi kuna kipindi tulikuwa na msanii mmoja tu Mabeste for like 4 years, ni kwa sababu tunaangalia talent.


“Na kusema kwamba sasa hivi tutakuwa hatujarudi nyuma utakuwa ni uongo, kuondoka kwao ndio tutarudi nyuma steps kadhaa, lakini pia kutokana kwamba plans tulizopanga kufanya wakati tukiwa nao zilikuwa hazijafika kuiva, we are ready to do that with someone else, Mungu hajagawa kipaji kwa watu wawili au watatu.”


Amesema anaamini baada ya Gosby, Vanessa, na Mabeste watakuja watu wengine ambao wana vipaji pia.


Kauli ambayo inaungana na ile ya Hermy B kuwa B’Hits itatangaza wasanii wapya wa label hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.


Tovuti ya Times fm ilitaka kufahamu kutoka kwa mwana sheria huyo kuhusu mkataba kati ya B’Hitz na wasanii hao na damages/athari za kuvunja mkataba huo zikoje na iwapo watawadai wasanii hao.


Amesema mikataba ilikuwa tight lakini kwa mazingira ya Tanzania na hali halisi ya kipato cha wasanii wa Tanzania hiyo mikataba inakuwa kama useless kwa kuwa kiasi kinachotakiwa kulipwa na msanii huyo ni kikubwa kuliko hali halisi ya maisha ya msanii husika.


“Ukimchukua bwana mti ukampeleka mahakamani, mahakama inaangalia damage ambayo imeingia katika kampuni, na mwisho wa siku inachukua maamuzi ambapo itakwambia bwana mti kama amepatikana na kosa amlipe bwana jose million 150 Kwa mfano, haimfungi. Problem ni kwamba bwana mti hana hata shilling 200 mfukoni mwake, we unadhani utamfanyaje bwana mti?” Alieleza kwa mfano.


“Kwa sababu mahakama ikishakupa judgement inakuacha ukatafute hiyo hela, haimfungi mtu. Kesi za madai sio kesi za jinai..sasa hapo imagine hapo ni wasanii wangapi leo unawafanyia kazi ya million 40 Million 50, ambayo ukiingia katika intellectual property court (mahakama ya maswala ya copy right), na copy right ni very expensive, tunaongelea six figures, eight figures. Sasa angalia ni wasanii wangapi hapa Tanzania wanaweza kukulipa eight figures.?” Amesema.


Kutokana na hali hiyo amesisitiza kuwa kuna haja ya kuwalipa wasanii pesa nyingi katika kazi zao huko wanakoenda kufanya ili wanapopata matatizo waweze kulipa, na kwamba bila hivyo mikataba ya label na wasanii Tanzania itakuwa useless.


Hii inamaanisha kuwa hakuna hatua zozote za kisheria ambazo B’hits itachukua kudai fidia kutoka kwa wasanii hao.


Hata hivyo uongozi wa B’Hits umesema utaachia nyimbo nyingine za wasanii hao zilizoko studio na kwamba zitachezwa redioni, lakini wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia kwa kuwa ni mali halali ya kampuni hiyo.


Msikilize hapa Amani Joachim:

No comments:

Post a Comment