Blogger Widgets

November 5, 2013

Baadhi ya Picha Zilisababisha Video Ya Sugua Gaga kuvunja rekodi ya video zake zilizopita kwa kutazamwa mara 20,000 ndani ya siku 3

http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2013/11/shaa-gaga.jpg
Mafanikio ya kazi mpya ya member wa zamani wa Wakilisha Sarah Kaisi aka Shaa yameanza kuonekana mapema kutokana na mapokeo mazuri aliyoyapata katika kipindi kifupi toka wimbo wake mpya ‘Sugua Gaga’ utoke wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Shaa mwenyewe, video ya ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi iliyowekwa na video zake zote zilizopita ikiwemo ‘LavaLava’, kwa kutazamwa mara 20,000 ndani ya siku tatu toka iwekwe youtube September 31.
“shaa_tz Oyooooooo its official.. #SuguaGaga imevunja rekodi ya #LavaLava na single zangu zote… #20,000hits on Youtube ndani ya siku3 tu! #shidaaaaa Nawashukuru wote.. #TeamShaa”
Shaa alishare mafanikio hayo Instagram jana.
Mpaka sasa video hiyo ambayo imefanyika Magomeni, Dar es salaam imefikisha hits 28,653 ikiwa ni siku 5 toka imewekwa youtube.

Sugua Gaga ni kazi ya kwanza kutoka kwa Shaa chini ya mkataba aliosaini na ‘Mkubwa na Wanae’ ya Said Fella kwa lengo la kumsimamia kwa miezi sita huku wakifanya nyimbo zitakazowalenga watu wa hali ya kawaida kabisa ambao nyimbo zake za mwanzo zimekuwa zikiwabagua.