Blogger Widgets

November 21, 2013

Babu Seya na Papii Kocha washindwa rufaa, kuendelea na kifungo cha maisha jela

Muimbaji mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo.
kkk
Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam.

Wawili hao wamewahi kukata rufaa tena na hawakufanikiwa na hukumu hii ya rufaa ni ya mwisho kusikilizwa. Katika rufaa hiyo wakili wa Babu Seya na Papii Kocha alikuwa akiiomba mahakama hiyo ifute ushahidi na waachiwe huru.