Sabrina Abdul
ndilo jina alilopewa na wazazi wake lakini yeye hupenda kujiita CUTE
BINAH, ni mtoto wa kwanza katika familia yake kati ya watoto wawili
waliozaliwa na mzee Abdul. Sabrina na video model ambaye anapenda sana
kazi hiyo na mbali na kuwa video model tu huwa anafanya kazi zake
nyingine ndogo ndogo zakusukuma maisha.
Unaweza
kujiuliza mtoto huyu mkali ameonekana wapi au unaweza ukawa umemuona
lakini usikumbuke ni video gani umemwona ya msanii wa hapa Tanzania.
Basi bwana huyu mrembo anaonekana kwenye video mpya ya HEMEDY PHD wimbo
wake wa REST OF MY LIFE. Mwanadada amecheza part yake vizuri kabisa na
asilimia 80 ameifanya video ile kuonekana nzuri kabisa.
Kama utabishana na mimi hebu fanya mpango wakubonyeza hii link ya video hiyo halafu utanipa jibu http://www.youtube.com/watch?v=fphCCywaunk
Nilimuuliza
Sabrina kwa mara ya kwanza wazazi kuiona video hii walisemaje na yeye
alinijibu ya kuwa aliwaaga kuwa anaenda kushoot video so haikuwa ngumu
sana walipoiona halafu isitoshe ile ndio kazi anayoipenda.
Nilimuuliza swala
la usumbufu wa wanaume toka alivyoonekana kwenye hiyo video ya Hemedy
au labda kama rafiki yake wakiume alimaindi akanijibu rafiki yake
wakiume anatambua kama ile ni kazi kwahiyo hawezi maindi ila kusumbuliwa
na wanaume ni kawaida mimi ni mtoto wa kike halafu isitoshe ni mzuri
najitambua.
From:Djchoka
No comments:
Post a Comment