Blogger Widgets

November 8, 2013

Habari Mbaya Kuhusu Msanii SHAA Wa Tanzania Hii Ni siku Chache Baad ya Kuachia Video Yake Mpya SuguGaga

Ikiwa ni siku nane toka video ya wimbo mpya wa Shaa ‘Sugua Gaga’ imeachiwa rasmi wiki iliyopita, video hiyo imeondolewa katika mtandao wa Youtube kwa madai ya kukiuka masharti ya haki miliki ya mtandao huo.
shaa sugua gaga
Hivi sasa unapotaka kuitazama video hiyo ya ‘Sugua Gaga’ iliyowekwa katika channel ya Shaa (ShaaMusicTV) pamoja na channel za watumiaji wengine inaleta ujumbe huu:
“This video contains content from Calif Entertainment Africa, who has blocked it on copy rights grounds”.

Akizungumza na Bongo5 muda mfupi uliopita Said Fella wa Mkubwa na Wanae ambaye ndiye anahusika na project hiyo, amesema hata wao wameshangazwa na kufutwa kwa video hiyo na kwamba wanajaribu kufuatilia kujua chanzo cha tatizo na aliyehusika.

Video hiyo iliyokuwa imevunja rekodi za video zote za Shaa kwa kutazamwa mara 20,000 ndani ya siku 3 toka imewekwa, mpaka Jumanne ya wiki hii ilikuwa imefikisha views 28,653.
www.youtube.com/watch?v=-KatIYYskF8