Blogger Widgets

November 22, 2013

Hii Hapa Story Kamili Kuhusu Lile Sakata la JB kufumaniwa na Mke wa Mtu Gest

LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa utata.
 
Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’.
Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah. Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku. Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa. Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake. Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
 “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”
Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.

No comments:

Post a Comment