Blogger Widgets

November 18, 2013

Huu Ndio Muda Wako wa Kuangalia Matukio Yote yayalijiri kwenye Arobaini ya Marehemu Alberty Mangwea

DSC01553 
Kila tarehe 16nov hua ni siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa ndugu yetu/mpendwa wetu Albert Mangwea,ambae alizaliwa huko songea mwaka 1982.Baadae wazazi kuhamia morogoro. Shughuli ya kukumbuka siku yake ya kuzaliwa imeambatana na siku ya kuhitimisha msiba yaani 40,katika kuelekea siku hii nyumbani kwao kihonda mkoani morogoro waliandaa misa ya kumuombea ambayo ilianza na mkesha wa tarehe 15 kuamkia 16 hizi ni picha za usiku wa mkesha nyumbani kwao albert.
DSC01453 
Hawa ni wana kwaya wakiendelea kuimba nyimbo mbali mbali za maombolezo
DSC01447 
Hawa ni miongon wa waliohudhuria akiwemo Bdozen toka xxl ya cloudsfm,Young Dee na Dj venture
Asubuhi kulipokucha tulielekea kanisani ambalo lipo barabara ya kuelekea Dodoma kanisa la ROMAN CATHOLIC mtakatifu Monica parokia ya Kihonda,Misa ilianza sa 1 asubuhi na iliongozwa na paroko wa kanisa hiloPadri OCTAVIAN MSIMBE.

DSC01479 
Misa ilipokamilika waumini wote tulisogea eneo alipolala mpendwa wetu ALBERT MANGWEA,ambapo tulipofika eneo la makaburini tulianza kwa kuelekea kaburi alilolala baba mzazi wa ALBERT MANGWEA mzee KENETH MANGWEA bbada ya misa kukamilika tulihamia kaburi alilolala mpendwa wetu/ndugu yetuALBERT MANGWEA ambalo lipo mita chache na la BABA.
DSC01489 
Misa ikiendelea kwenye kaburi la marehemu mzee KENETH MANGWEHA baba mzazi wa Marehemu Ngwea.Mara baada ya kukamilika kwa misa kwenye kaburi la mzee Keneth waumini wote tuliokuwa makaburini tulisogea kwenye kaburi alilolala mpendwa wetu MANGWEA
DSC01496 
Misa ikiendelea kwenye kaburi la MANGWEA
DSC01499 
Waombolezaji wakifatilia ibada.Misa ilipoisha watu wengi waliokua karibu,wapendwa wa ALBERT hawakuondoka mapema makaburini ndugu/mzazi walitangulia nyumbani lakini watu wengi waliokaribu waliendelea kuwa makaburin wakiwasha mshumaa kama ishara ya kumkumbuka mpendwa wetu na kumsalia huko aliko apumzke kwa aman
DSC01514 
Kutoka kushoto ni M2the p,Darkie Master,Quick Rocker,Dj Venture na Dulah spatan,na kulia ni Bdozen,Geez Mabovu na nndugu waliokua karibu na ngwair wakisali kwenye kaburi la mpendwa ALBERT MANGWEA.
DSC01519 
Mama mzazi wa Marehemu Ngwea akiweka shada la maua kwenye kaburi la NGWEA.
DSC01550 
Bdozen akiwasha mshumaa.
DSC01560 
Young Dee nae akiwasha mshumaa juu ya kaburi la NGWEA.
DSC01552 
Darkie Master akipiga saluti kwenye kaburi la Ngwea.Baada ya kuwasha mishumaa na kuweka mashada ya maua,kilichofuata zilikua zikisikika nyimbo za Marehem ngwea ambazo zilikua zikipigwa kutoka kwa gari ya maneck nyimbo hizo ni zile ambazo hazikutoka japo zipo tayari studio,watu waliokua eneo hili ni pamoja na Quick Rocker,Maneck,Bdozen,Young Dee,Dark master,Geez mabovu,Dj venture[ambae aliwahi kuwa meneja wa ngwea]Dulah spatan,ndg Muro junior Aliyekua meneja wa Ngwea had kipindi cha mwisho ,Jordan moja ya wadogo wa ngwea kimuzik aliokua akiwasimamia chin ya lebel yao ya DENJAVUU MUSIC.
DSC01570 
Hapa ni nyumbani kwa ndugu yetu ALBERT MANGWEA.DSC01589 
Muziki wa taratibu pamoja na nyimbo za Ngwea zilikua zikiendelea kutawala.
DSC01578
Ama kwa hakika NGWEA alikua mtu wa watu.MUNGU ailaze roho yake mahali pema peponi,Amin