Blogger Widgets

November 4, 2013

Jinsi Mh Rais Jakaya Kikwete naMakamu wa Rais Dr. Bilali walivyofunga Safari Kwenda Kumjulia Hali DKT.SENGINDO MVUNGI katika Hospitali ya Muhimbili


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia na daktari wa zamu wakimwangalia Mjumbe wa Tume ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha Mifupa (MOI) jana Oktoba 3, 2013 kufuatia kujeruhiwa kwake na watu wanaosadikiwa ni majambazi usiku wa Jumamosi Oktoba 2, 2013. 
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Dkt. Mugisha Clement, aliyekuwa akimpa maelezo kuhusu alivyompokea Mjumbe wa Tume ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, aliyelazwa katika Kitengo cha Uangalizi Maalum (ICU) MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, wakati alipokwenda kumjulia hali, kufuatia kujeruhiwa na majambazi usiku wa kuamkia jumapili huko nyumbani kwake maeneo ya Kibamba. Picha na OMR