Blogger Widgets

November 13, 2013

Kama Ulikuwa Hujui Maana ya Tatto alizochora Ney wa Mitego Soma Hapa AlichoelezeaMuziki na sanaa ni ubunifu na wala si kujua kuimba tu!. Wiki iliyopita nilimnukuu mzalishaji mkongwe wa muziki hapa nchini Master J akisema idadi kubwa ya wasanii hapa bongo wanafanikiwa si kwa sababu wanaimba vizuri tu bali pia wanavutia pale wanapokuwa jukwaani.
Kwa tafsiri hiyo ina maanisha msanii ni muhimu kubeba dhana nzima ya sanaa na kuonekana wa tofauti popote pale anapoonekana.

Ney wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii wabishi wanaofanya muziki mgumu maarufu kama Hip Hop, ambaye amejaribu kubeba dhana hiyo kama msanii anayetafsirika kimwonekano.

Wiki hii gazeti moja limezungumza na Ney kuhusu ‘michoro yake ya ‘Tattoo’ katika maeneo mbalimbali ya mwilini.

Ney anasema ‘tattoo’ hizo ametengeneza miaka miwili iliyopita huku akibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kuchora michoro hiyo.

“Nimeanza kuchora tangu 2002 nikiwa kidato cha pili katika Sekondari ya Mbenzi Beach, na ilikuwa kipindi ambacho nina ‘haso’(nina hangaika) kufanikiwa kimuziki katika uamuzi huo haikutokea bahati mbaya kufanya hivyo,” anasema.

Zina tafsiri kimaisha

Katika michoro ya ‘tatoo’ alichora mwilini kwa sasa Ney anasema zina tafsiri mbalimbali katika maisha yake. Anaongeza kuwa katika tatoo hizo zipo ambazo hazitafutika milele.

“Lakini pia kuna ambazo zinaweza kufutika, kaka yangu alinishauri na kueleza katika uchoraji wa ‘tattoo’ hizo, kwa sasa hivi ninayo michoro mitatu yenye tafsiri kubwa katika maisha yangu,” anasema Ney.

Anasema mkono wa kulia kuna ‘tattoo’ yenye Nanga ya Hip Hop ikiwa na maana kuwa yeye ni mtu mwenye imani na ndoto za kufanikiwa kupitia muziki huo wa ‘Hip Hop’.

Anasema ‘tattoo’ iliyopo katika mkono wa kushoto ni nyoka mwenye mabawa(Dragon) ,kiumbe ambacho ni adimu kuonekana duniani.

“Maana ya nyoka huyu inamaanisha mimi ni mtu ghari na adimu duniani, siku zote huwa najikubali sana na kuamini mimi ni mimi na hakuna anayeweza kuwa kama mimi duniani kote, ndiyo maana ya kuchora ‘tattoo’ hiyo,” anasema Ney.