Blogger Widgets

November 4, 2013

Picha: Lady Gaga avaa kama zombie kwenye tuzo za YouTube, apigwa chini na mpenzi wake sababu ya ubusy usioisha

Jumapili hii Lady Gaga aliendeleza mtindo wake wa kuvaa nguo za ajabu ajabu. Kwenye tuzo za Youtube zilizofanyika Jumapili hii huko New York City, staa huyo alionekana amevaa shati jeusi, bila suruali na huku akiwa ameweka meno ya bandia yaliyotokeza nje.
article-2483175-192D4E1800000578-321_634x952
Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa Lady Gaga ameachwa na mpenzi wake Taylor Kinney. Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, uhusiano kati ya Gaga na muigizaji huyo umekuwa matatani kwa miezi kadhaa kutokana na Lady Gaga kuwa busy kupitiliza.
article-2486849-192D98F900000578-683_634x804

‘Taylor amemuambia Gaga kuwa ameolewa na kazi yake na hawezi kuwa na uhusiano na staa huyo pamoja na jinsi anavyohangaika kujionesha,’ chanzo kimoja kililiambia gazeti hilo.
Gaga-Taylor-Kinney-Doube-Date-Night
‘Anampenda sana lakini humuona kwa nadra sana. Gaga huwa hasimami kufanya kazi- huandika nyimbo akiwa anaoga na huota nguo mpya za kuvaa akiwa amelala.’
Kinney, 32, anasemekana kuchanganyikiwa na kuwa peke yake mara nyingi na muda mchache wa kukaa na Gaga, ambaye mara zote huwa amezungukwa na wasaidizi kibao pamoja na walinzi. Wapenzi hao huwa na usiku mmoja tu ndani ya mwezi mzima wa kuwa pamoja.
From:Bongo5