Blogger Widgets

November 12, 2013

PICHA:Irine Uwoya Aanza Mazoezi ya Kupunguza Mwili wake Akiwa anafanya Mazoezi na Rashid Matumla

Irene Uwoya ameamua uanza mazoezi ya kupunguza unene na kujiweka fiti na kurudisha mvuto wake wa awali ambao unadaiwa kupotea mara baada ya kujifungua huku media na wataalamu wa fashion wakimuandama mara kwa mara kuwa kapoteza mvuto wa mwanzo kwa kujiachia kunenepeana kiasi cha kupoteza mvuto. Owoya yupo chini ya mwalimu wake wa mazoezi Rashid Matumla ambaye ni bondia maarufu nchini na pia wanakuja na filamu wakiwa pamoja ambayo inaitwa Raundi Ya 8.
"Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili


unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe"

 Filamu hiyo imeshutiwa Tanga, Dar es salaam na Morogoro huku waigizaji wengine wakiwa ni Francis Cheka na Lumolwe Matovolwa.

Uwoya akiwa na Rashid Matumla....................