Blogger Widgets

November 8, 2013

Soma Skendo Nyingine Aliyoipata Msanii Wa Bongo Movie Rayuu a.k.a Mama Tatoo Akihusishwa na Jackyne wolper


Rayuu anadaiwa kuiga fashions za nywele za star mwenzake wa Swahiliwood Jackline Wolper. Chanzo kimoja ambacho kipo karibu na Rayuu kimeitonya Swahiliworldplanet kwa kusema "Rayuu siku hizi anataka kuwa copy ya Wolper sijui, si mmeona siku hizi yuko busy kumuiga wolper mitindo ya nywele ha ha ha haaa ustaa kazi jamani!" kilisema chanzo hicho huku kikiangua kicheko cha haja.

Baada ya kupata habari hizo ilibidi
Swahiliworldplanet  kumtafuta Rayuu na alipopatikana na kuelezwa kuhusu habari za kuwa busy kumuiga Wolper fashion za nywele kwanza aliangua kicheko pia na kujibu "ha ha ha ha haa.... huo ni uzushi, kwanza mimi sipo karibu na yeye(Wolper) sasa ntajuaje styles zake jamani? mi huwa naangalia styles za Rihanna ndiyo nabadilisha kinatokea kitu kingine ambacho ni tofauti na Rihanna, mi najidizainia mwenyewe styles zangu na nina saloon yangu ndo huwa wananitengeneza"
                                                            Rayuu