Blogger Widgets

November 13, 2013

Story Iliyomake Head Line Sana Leo Ni Hii Kuhusu Mainda na Ray Pia Utoaji wa Mimba Ndio Imekuwa Gumzo

Mainda
Mainda ambaye ni msanii maarufu na wa siku nyingi Swahiliwood kwa mara ya kwanza amefungukia uhusiano wake na Vicent Kigosi(Ray) baada ya penzi lake na Ray kuvamiwa na Chuchu Hans na Johari. Mainda pia alisema aliwahi kutoa mimba ya Ray na walidumu katika uhusiano wao kwa miaka 9 kabla ya Johari na Chuchu kumharibia. Mainda aliyasema hayo katika exclusive interview na mtandao maarufu kwa skendo za mastaa hasa wa filamu Globalpublishers kupitia gazeti la Risasi. Soma mahojiano ya Mainda na mtandao huo...

Risasi: Baada ya kifo cha Maxi, Ray alijitokeza na kukutongoza au siyo?
Mainda: Hapana, nakumbuka ilikuwa Siku ya Valentine’s Day mwaka 2004...sikumbuki kama tulitongozana ama vipi lakini ilitokea tukajikuta kwenye uhusiano.
Risasi: Umedumu kwa muda gani katika uhusiano wako na Ray?
Mainda: Miaka tisa, nilimpenda sana hata yeye alikuwa akinipenda na kuniheshimu sana.
Risasi: Kwa nini mmeachana?
Mainda: Hajaniacha wala hatujaachana. Miye ndiye nimemwacha.
Risasi: Jeuri ya kumuacha Ray umeitoa wapi?
Mainda: Siyo jeuri, ni kujiamini na kujitambua tu.
Risasi: Chanzo cha kumuacha nini labda?
Mainda: Nilipojihakikishia kwamba anatoka na Chuchu Hans na Johari, nikafanya uamuzi.
Risasi: Lini ulipata uhakika huo?
Mainda: Ni hivi karibuni. Niliumia sana (analia).
Risasi: Pole sana, jikaze tafadhali. Siku zote ulikuwa hujui?
Mainda: Nilikuwa nasikia tu maneno, lakini nilipothibitisha nikaamua kukaa pembeni.
Risasi: Uhusiano wako na Ray ulifikia hatua gani?

Mainda: Mwaka 2009 miye na Ray tulienda kanisani kwa ajili ya kutaka kufunga ndoa. Kwa sababu  mwenzangu ni Mkatoliki ilibidi aokoke na kunifuata kwenye wokovu ili tuweze kufunga ndoa yetu, nashangaa amebadilika tena.
Risasi: Ulibadili dini kwa ajili yake?
Mainda: Big no! (Hapana kabisa) ulikuwa ni uamuzi wangu binafsi.
Risasi: Mipango yenu ya ndoa ilikuwaje?
Mainda: Tulipanga kufanya private wedding (ndoa ya siri).
Risasi: Unauzungumziaje uhusiano wako na Ray? Namaanisha ni nini hasa ambacho hakitaweza kufutika kirahisi katika kumbukumbu zako?
Mainda: Daah! (anavuta pumzi ndefu kisha anazishusha) Nilimpenda sana Ray. Ilifikia hatua nikapata mimba yake. Mapenzi yetu yakaongezeka lakini kwa bahati mbaya ilitunga nje ya kizazi na ilinitesa sana, tena kwa kuwa ilikuwa ni mimba ya kwanza sikuwa nimejitambua mapema. Madaktari wakashauri niitoe, nikakubaliana nao.
Risasi: Ilikuwa ni mwaka gani?
Mainda: Sikumbuki, ila ni kipindi tulipokuwa tukirekodi filamu iitwayo Johari (kwa kumbukumbu za Risasi ni mwaka 2005).
Risasi: Kuna madai kwamba wewe hukubaliki kwa mama yake Ray, ambaye anadaiwa anamkubali zaidi Johari, ni kweli?
Mainda: Siwezi kumsema vibaya yule mama, namheshimu sana lakini inawezekana kuna maneno ya uongo ambayo ameambiwa na watu.
Risasi: Kama yapi?
Mainda: Kuhusu miye kuwa na Ukimwi. Ngoja nikuambie kitu kaka’ngu, baada ya kifo cha Maxi, watu wengi walininyooshea vidole kwa kuamini kuwa Maxi amekufa kwa ugonjwa huo jambo ambalo siyo la kweli. Nakumbuka mwaka 2003, nilienda na Maxi Mwananyamala (Hospitali), alitolewa vipimo vingi (kikiwemo cha VVU), akabainika kuwa na kansa ya damu.
Akatakiwa kwenda Ocean Road (Hospitali) ambako walipendekeza akatwe mguu uliokuwa umeathirika na ugonjwa huo lakini alikataa. Alisema ni heri afe kwa ugonjwa huo kuliko kuzikwa akiwa na upungufu wa viungo mwilini mwake.
Risasi: Kuna tiba alishaanza kuitumia Ocean Road kabla ya kifo chake?
Mainda: Yeah! Alikuwa akichomwa mionzi, hadi kifo kilipomfika.
Risasi: Pole sana.
Mainda: Ahsante... ila baada ya kifo chake, watu wengi walihisi amekufa kwa Ukimwi na wakaamini nami pia ni mwathirika... hiyo hali ilinitesa sana (anaangua kilio).
Risasi: Pole sana, usilie...jikaze tafadhali.
Mainda: Kama kweli Maxi angekuwa amekufa kwa Ukimwi, Ray asingekubali kuwa na mimi kwa sababu  alikuwa rafiki yake na alishiriki kumuuguza kwa kiasi kikubwa.
Risasi: Kwa hiyo unaamini kwamba mama Ray alipandikizwa sumu hiyo?
Mainda: Binafsi nilikuwa simfuatilii ila mwanaye alijitahidi kuniweka karibu na mama yake.
Risasi: Kivipi?
Mainda: Mara kadhaa Ray alikuwa akinipigia simu na kunitaka niongee na mama yake au ndugu zake, aliniweka karibu sana na familia yake.
Risasi: Umewahi kupima Ukimwi?
Mainda: Siyo mara moja, baada ya maneno hayo,  mwanzo nilipima kwa hofu kwa kuhisi labda wale madaktari wa Mwananyamala walinidanganya kwa vile nilikuwa mdogo.
Risasi: Majibu yako yanasomekaje?
Mainda: Namshukuru Mungu, nipo negative (hana uambukizo).
Risasi: Ulijisikiaje ulipogundua kuwa Ray anatembea na Johari na Chuchu?
Mainda: Awali sikujua na kila nilipomuuliza Ray alinikatalia.
Risasi: Kwa hiyo ulimwamini Ray?
Mainda: Sana, tena nilipokuwa naye alikuwa akiwapigia na kuweka loud speaker kisha kuwauliza kama walikuwa wapenzi, walikataa.
Risasi: Unawachukuliaje Johari na Chuchu?

 Soma zaidi interview hii hapa Globalpublishers kujua zaidi aliyofunguka Mainda