Blogger Widgets

November 10, 2013

KeshoKuna Story Itawaijia Juu ya Huyu Mume wa Mtu alivyonusurika Kuuwawa na Huyu Changudoa Mwenge Siku Kadhaa Zilizopita

Hatoki mtu hapa: Joseph Hussein akiburuzana na kimada wake Neema Samson baada ya kudaiwa kupenda vya bure.
WAKATI Oparesheni Fichua Maovu katika jamii inayoendeshwa na Global   ikiwa kazini, wikiendi iliyopita ilinasa timbwili zito la aina yake kwa mwaka 2013 ambapo mume wa mtu, Joseph Hussein (31), nusura auawe na kimada..
Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge, Dar mishale ya saa 10 usiku ambapo mwanaume huyo, mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Neema Samson, mkazi wa Buguruni.

  Lazima unipe changu: Neema Samson akiwa amemkaba mteja wake baada ya kushindwa kumlipa chake.

Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama wanavyokubaliana.Starehe gharama: Joseph akizidi kupewa hali ngumu na Neema, pembeni wananchi wakianza kusogea eneo la tukio.
SEKESEKE LAFUNGA MTAA
Kutokana na sekeseke hilo la kupigana, watu kibao walitoka nje ya nyumba zao na kushuhudia kilichotokea ambapo walipigwa na butwaa huku wakilalamika kuwa waliamshwa usingizini na watu waliokuwa kwenye starehe zao.
WAAMKA NA BOKSA, NIGHTDRESS
Huku wakiwa na boksa, night dress, vipensi na wengine mataulo, majirani wa eneo hilo walimshuhudia Neema akiwa amemkaba Joseph shingoni hadi akashindwa kupumua na kusababisha hekaheka mtaa mzima.

“Kha! Mwanamke amemkaba mwanaume anataka kumuua kisa ni nini?” alihoji mmoja wa majirani hao.

Neema alikuwa akimnyonga Joseph kwa kutumia fulana yake akilalama kuwa amezoea kupewa penzi kisha kuingia mitini bila kulipa.

“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa hasira.

Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu yake aina ya Nokia.

MJUMBE ATEMA CHECHE
Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti, alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema.

  Baada ya wananchi kuona wapenzi hao wanazidi kuvuruga amani mtaani kwao, waliamua kuwaweka mtu kati tayari kuwapeleka sehemu husika.

SOO HILOOO POLISI
Wawili hao waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema waliposhirikiana kuwabeba kisha kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo cha polisi....

Safari kuelekea kituo cha polisi: Wananchi wakiwabeba msobemsobe kuwapandisha kwenye Bajaj tayari kuelekea kituo cha polisi.