Blogger Widgets

November 5, 2013

Tazama Jinsi Msanii wa Bongo Movie Batuli Alivyowekwa Kati na Fans Wake

URAFIKI
Dada Batuli nataka tuwe marafiki wa ukweli unifundishe uigizaji. George, Dar, 0656314282
BATULI: Nikisema mimi nitakufundisha sanaa nitakuwa nakudanganya, nenda kwenye vikundi mbalimbali vya sanaa ujifunze utaweza tu.


HUYU KAINGIA CHAKA
Nje ya fani najua ulikuwa na mgahawa wa maziwa maeneo ya Mwembe-Chai Magomeni, Dar. Wewe ni mzuri, una miguu mizuri ya bia, nakukubali sana. Msomaji, 0712958578
BATULI: Hapana sijawahi kuwa na mgahawa, asante kwa kunikubali.
 
ELIMU VIPI?
Batuli uko vizuri kwenye sanaa, nakukubali sana ila ningependa kujua kiwango chako cha elimu na umesomea wapi? Ibra Haidhuru, Morogoro, 0712551441
BATULI: Nina elimu ya sekondari na nimesoma Mwanza, Dar na Arusha.
ANATAKA KUMUWEKA NDANI
Mtoto mzuri kama wewe nikiamua kukuweka ndani utatulia kweli? Msomaji, 0714452023
BATULI: Mimi ni mtafutaji, siwezi kukaa ndani. Kuhusu kutulia mimi nimetulia sana.

MAPENZI
Batuli uko poa kiukweli unajua, vipi yule mpenzi wako wa kitambo analalama umemkacha kisa wewe staa. Shadee Sharif, Dar, 0713815145
BATULI: Siyo kweli, mimi sijamkacha mpenzi yeyote.
MATARAJIO
Dada Batuli nakukubali sana katika kazi zako, ningependa kujua matarajio yako ya baadaye kupitia sanaa. Msomaji, 0789090479
BATULI: Matarajio yangu ni kujitangaza kimataifa zaidi.

NJE YA FANI

Mbali na sanaa unashughulika na kazi gani?  Selestini Jaston Mmassy, Tanga, 0713955904
BATULI: Mimi ni Balozi wa Amani Tanzania.

MAVAZI
Batuli umesoma katika shule yenye maadili ya Kiislamu, iweje unaigiza katika mavazi yasiyo na staha? Je, wazazi wako wanakuchukuliaje? Hidaya, Arusha, 0754556200
BATULI: Hii ni kuigiza tu na siyo maisha yangu na wazazi wangu wanajua pale nipo kazini.

HUYU ANA STORI
Nina stori ambayo unaweza kuitengenezea muvi, tuwasiliane nitakupatia bure. Zangira, Dar, 0655288044
BATULI: Asante sana.

HANA MPANGO NA
DIAMOND
Batuli nakukubali kwa kazi zako nzuri, eti nasikia ulishawahi kutoka kimapenzi na Diamond, je, ni kweli? Rama, Tanga, 0656907070
BATULI: Sijawahi kuwa na uhusiano na Diamond (Nasibu Abdul) na sina mpango huo.

SUALA LA MAVAZI TENA
Kiufupi msanii ni kioo cha jamii, nikiwa na maana kwamba kile anachokifanya msanii ndicho jamii inachojifunza kwa asilimia kubwa. Je, wewe kama msanii unalionaje hili suala la mavazi hasa ninyi wasanii wa kike mnaifundisha nini jamii? Msomaji, 0755143964
BATULI: Mtu unavyoigiza lazima uvae kutokana na filamu inavyosema ili kuleta uhalisia kama ni tofauti na filamu siwezi kuwazungumzia kwa sababu mimi sipo hivyo.

MAADILI

Batuli ni kwa nini baadhi ya waigizaji maadili yenu yapo tofauti na ya Kitanzania? Iddi Mayunga, Dar, 0766185177
BATULI: Stori za filamu ndizo zinatufanya tuvae hivyo. Pia hapa ni mjini huwezi kuvaa kama uko kijijini hivyo tunabadilika kutokana na mazingira.

OMBI
Batuli wewe ni mrembo kuliko msanii yeyote, naomba uwe mpenzi wangu kama inawezekana chukua namba yangu tafadhali. Gerald, Arusha, 0754046004
BATULI: Asante.