Blogger Widgets

November 6, 2013

Tazama Picha Jinsi Indonesia wanavyofanyiwa "Massage" Kwa Kutumia Nyoka Mkubwa

Unapenda kufanyiwa massage na nyoka? Unaweza kukaza roho na usiogope kung’atwa? Kama ndio basi nenda nchini Indonesia utaipata kwa raha zako.
snake-spa-2
Massage hiyo inapatikana Bali Heritage Reflexology and Spa huko Jakarta, Indonesia ambako wanaweza kukuondolea uchovu wako wa siku nzima kwa massage ya nguvu inayofanywa na nyoka mkubwa.
snake-spa-1

Massage hiyo inafanyika kwa nyoka huyo kuwekwa juu ya mwili wa mteja na mengine huachiwa yeye nyoka afanya yake. Ili kupata huduma hii mteja hutakiwa kulipa dola 47 ambazo ni zaidi ya shilingi 76,000 za Tanzania.