Blogger Widgets

November 1, 2013

UJIO WA BABY MADAHA:kuja na filamu yake ya ‘The Gal Bladder’ chini ya Candy n Candy.Tazama Picha

Msanii Baby Madaha kutoka Tanzania ambaye kwasasa yuko chini ya label ya Candy n Candy ya Kenya, baada ya kutoa video yake mpya sasa anatarajiwa kuja na filamu mpya ya Kiswahili ‘The Gal Bladder’.
baby madaha movie
Kwa mujibu wa mtandao wa GHAFLA wa Kenya, filamu hiyo inaweza kuachiwa hivi karibuni. Baby Madaha amekuwa katika headlines mfululizo kwa siku za karibuni kutokana na mambo mengi anayoyafanya, kitu kinachoashiria matunda ya mkataba wake na Candy n Candy.

baby madaha

Hivi karibuni msanii huyo amezindua begi ndogo za kubebea zawadi ‘gift bags’ zenye picha yake, na aliiambia tovuti ya TIMES FM kuwa mradi wake utakaofuata ana mpango wa kuja na vifaa vya watoto kama toys.