Blogger Widgets

December 18, 2013

Duh! Kanye West afanya Maajabu kwa kundi la watu wanaomfanyia make-up Kim Kardashian

Linapokuja suala la kuhakikisha mama wa mwanae, North anapendeza kadri iwezekanavyo, Yeezy hana mkono wa birika. Na ndio maana ametema $250,000 (zaidi ya shilingi milioni 400) kwaajili ya kundi la watu wanaompamba Kim Kardashian ( glam squad).
article-0-1A29E6FC00000578-403_634x971
Staa huyo amekuwa akisindikizwa na mchumba wake kwenye ziara yake Yeezus nchini Marekani na amehakikisha mtu wa kumpamba nywele Kim (hair dresser) msanii wa make-up na mtu wa mitindo kuitwa muda wowote na mahali popote wanapohitajika kumpamba mrembo huyo kwakuwa amekataa kutumia watu wengine.

Chanzo kimeuambia mtandao wa RadarOnline.com: ‘Kanye amemuambia Kim atatumia kiasi chochote kuufanya muonekano wake tayari kwa upigaji picha mkubwa muda wowote akitaka Hivyo hair stylist wa Kim, make-up artist na mtu wa mitindo wote wanaoishi Los Angeles, wako tayari saa 24/7, kuchukua private jet kumfuata alipo.

“Kim anaamini timu yake pekee kumfanya apendeze na hataki kufanya kazi na watu wa nje. Hii si rahisi na Kanye ametoa $250,000 wakati yupo kwenye ziara kwaajili hiyo. Pesa haina maana yoyote kwa Kanye sababu anataka mrembo wake aonekane bomba,” kilisema chanzo hicho.
Inadaiwa kuwa Kanye hachukizwi na matumizi makubwa ya Kim sababu yeye mwenyewe hutumia fedha nyingi mno kwaajili yake.