Blogger Widgets

December 10, 2013

Imekuwa Kama Fashion:Tazama Picha za Dada Aliyechaniwa Nguo na Kutaka kubakwa Baada ya Kusadikiwa kuwa katembea Nusu Uchi


Mrembo akilia baada ya kunusurika kubakwa
Mwanahabari akiwa katika Oparesheni ya Fichua Maovu inayoendeshwa na Magazeti ya Global Publishers, mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.
Wananchi wakiwa wamemzunguka
WAONESHA MAUNGO NYETI BILA ‘MAKUFULI’
Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta katika hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo wakaonja joto ya jiwe.
Akisaidiwa kuingia katika bajaj na wasamalia wema
WATOKA SINZA KUELEKEA MANZESE
Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda,  walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na Morogoro, Dar.
“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana hao.
 
WAJIFANYA JEURI
Mwendesha bodaboda mwingine aliliambia gazeti hili kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu
kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.

MATUSI NJENJE
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba
badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama kabisa.

MWENYE ‘MDOMO MCHAFU’ AKIONA
“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’
walimkamata na kumpa kichapo kikali.
“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa
ameshachaniwachaniwa nguo na ku... (hayaandikiki gazetini),” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake. CREDIT-GPL