Blogger Widgets

December 13, 2013

Kwa Wale Watumiaji wa Instagram Furahia Hii Huduma Mpya Iliyoanzishwa Jana

Kwa watumiaji wa Instagram, umeshawahi kuwa na picha unayohitaji kushare na mtu flani peke yake bila marafiki wengine kuiona, lakini ukashindwa kutokana na kutokuwa na huduma hiyo hapo awali? Instagram wameligundua hilo.
insta
Mtandao wa Instagram unaozidi kukua kwa kasi jana alhamisi (Dec 12) umetangaza kipengele kipya kwa watumiaji wake, ambao sasa wanaweza kutumiana picha, video na ujumbe moja kwa moja ‘Instagram Direct’.
Hapo Kabla mtumiaji wa Instagram alikuwa na uwezo wa kushare tu picha ambayo inaonekana kwa followers wake wote hivyo haikuwa na privacy, lakini kwa kipengele kipya cha ‘Instagram Direct’ mtu anaweza kuwatumia picha na video watu anaowataka kuanzia mtu mmoja hadi 15 na ni private.

“Wakati mwingine unahitaji kushare sio na kila mtu, lakini na kundi flani maalum” alisema Co-founder na chief executive wa Instagram Kevin Systrom , wakati wa utambulisho wa feature hiyo jijini New York jana.