Blogger Widgets

December 23, 2013

Soma Issue inayoendelea Kuhusu Hili Sakata la Avril wa Kenyakuwa kwenye uhusiano na mfanyabiashara wa Afrika Kusini sababu ya pesa

Habari ya ‘mujini’ Nairobi ni kuwa mwimbaji wa Kenya Avril Nyambura sasa ni mchumba wa mfanyabiashara tajiri wa Afrika Kusini ambaye ndiye anategemea kumuoa mwakani.
avril2
Baada ya taarifa juu ya kuchumbiwa kwa mrembo huyo wa Ogopa Djs ya Kenya kusambaa wiki chache zilizopita, Avril amekanusha uvumi ulioenea kuwa yuko kwenye uhusiano na mfanya biashara huyo kwasababu ya pesa.
“Tumefahamiana muda mrefu, kama ni kuhusu pesa ningekuwa naendesha Range Rover mwaka huu na nisingekuwa naishi South B. He is amazing, tunaelewana na sijali kile watu wasemacho”, alisema muimbaji wa Hakuna Yule, Avril.
Avrila amesema ndoa yao haitakuwa hivi karibuni kutokana na wao wote kutoka makabila tofauti mchumba wake ni Mzulu na Avril ni Mkikuyu, hivyo kuna taratibu za kitamaduni za kufuata “The wedding won’t be that soon. He is Zulu and I am Kikuyu, there are some cultural things involved,”.

Kwa sasa Avril na mumewe mtarajiwa wako Mombasa kwaajili ya kusheherekea Christmas, na baadaye wataelekea Johannesburg kwaajili ya kuupokea mwaka mpya.