Blogger Widgets

December 31, 2013

Soma Maneno ya Chege,Afande Sele,Belle 9,Nay wa Mitego, Young Killer na Madee wakiuelezea mwaka 2013 kimuziki

Wasanii wa muziki Chege, Afande Sele,Belle 9,Nay wa Mitego, Young Killer na Madee wamengufuka na kueleza jinsi muziki ulivyobadili maisha ya wasanii ndani ya mwaka 2013 pamoja na kiwanda chote cha muziki wa Tanzania. Hivi ndivyo walivyouelezea:
Nay
Nay Wa Mitego

Mwaka 2013 ni mwaka ambao umefanya mapinduzi ya vipato vya wasanii wengi. Katika maisha yangu kuna vitu kadhaa nimevifanya ambavyo sijawahi fanya katika miaka sita ama saba iliyopita ila mwaka 2013 vimetimia hata wananchi wameona show zimeongezeka mara huku mara kule yote ni mafanikio ya mwaka huu.
Kwaupande wa production ya muziki wangu mwaka 2013 umekuwa katika mawazo yangu,nimekuwa ni mtu wa kuumiza kichwa kuboresha aina ya muziki wangu,nimeweza zunguka Kenya,Uganda ili kutafuta ladha na ubunifu fulani katika muziki wangu. Muziki wa mwaka 2013 ni muziki tofauti na wa miaka yote iliyopita. Muziki wa 2013 umekuwa ni wa ushindani, kama ni video wasanii wanatoa video kwa ushindani. Wasanii wengi wamejaribu kuvuka mipaka ya Tanzania kutengeneza muziki wao,makampuni makubwa yanawatumia wasanii kujitangaza zaidi. Kwahiyo 2013 ni mwaka wa mafanikio,tunaomba Mungu 2014 iwe ni step nyingine kwenda mbele zaidi katika kila nyanja ya muziki.
Madee

Madee

Muziki wa mwaka 2013 kwa upande wa vipato vya wasanii, mimi nasema ni mwaka wa neema. Kama nilivyowahi kuwaambia wimbo wangu wa ‘Pombe yangu’ umeniingizia zaidi ya milioni 130 kwa mwaka huu. Kwahiyo kwa upande wangu mambo yako poa.
Kwenye production ya audio naona kama kumekuwa na changamoto kubwa sana kwa maproducer wakubwa. Maproducer wakubwa kidogo kama wamelala hivi na maproducer wadogo wakawa wametake industry. Lakini hii yote inatokana.. kuna kitu kimoja ambacho maproducer wakubwa walikuwa wamejiwekea, yaani unakuta sijui ni wavivu au wameridhika na ile kazi au walikuwa tayari walishabweteka kwa kuona kwamba hakuna mtu anaowakimbiza nyuma. Unajua kama haukimbuzwi hauwezi kimbia kwa nguvu,lakini ukiona mtu anakukimbiza unaweza kukimbia kwa nguvu. So sijui kama walikuwa wamebweteka ama wavivu au wa nini.Lakini maproducer wadogo wakawa wanafanya kazi usiku na mchana mpaka wasanii wakubwa wote wakawa wanakimbilia kwa maproducer wadogo. Ni baadhi tu ya maproducer wakubwa ambao wamejaribu kuendelea,wakatoa hits mbili tatu ambazo zimehit 2013. Lakini kiukweli maproducer wadogo walikuwa hot 2013. Hii inatokana maproducer wakubwa kuona kwamba wao wameshafanikiwa. Sitaki kuwataja majina lakini nikishaongea hivyo wenyewe wanajijua.
Chege

Chege

Malipo sio mabaya kwasasabu maisha yanaendelea,ni tofauti na kipindi cha nyuma. Kwahiyo sasa hivi kuna unafuu fulani. Sasa watu wanajenga nyumba,wanatembelea magari mazuri ,watu wanaishi vizuri na familia zao nafikiri tumetoka sehemu tulipokuwa tunasonga mbele. Production ya kazi za wasanii mwaka huu imekuwa kutokana na ushindani uliopo,wasanii wamekuwa wakifanya video kali na za gharama. Kwahiyo mimi naona 2013 ni mwaka wa mafanikio kwa wasanii pamoja na muziki wao.
Belle 9
Belle 9

Kwa upande wangu mimi, muziki wangu umeimprove kwasababu ukiangalia ngoma nilizofanya mwaka 2012 na ngoma ambazo nilizofanya mwaka 2013 nit ofauti. Ukiangalia ngoma kama ‘Listen’ niliachia mwanzo wa mwaka 2013,lakini imeniweka vizuri mpaka katikati ya mwaka naweza sema. Halafu mwisho wa mwaka nimeachia hii ‘Waniita’ lakini watu wameipokea vizuri sana ingawa nimeifanya tofauti ila imeleta matokeo makubwa mpaka sasa.
Kwa upande wa production zetu 2013 sijajua tatizo ni nini,sijui ni vifaa au watalam bado sijapata kujua tatizo nini mpaka tunashindwa kupiga hatua. Sio video wala audio bado sana,kuna nyimbo nyingine unaweza ukakuta ni nzuri ila production mbaya. Ukisikiliza kwa kuchambua huwezi elewa mpangilio wa vyombo. Ila kwa upande wangu, mwaka 2013 Tanzania tumefanya poa zaidi ya Kenya kwenye production ya video kwa wasanii wa Tanzania waliofanyia Kenya na hapa nchini. Kwahiyo tunapiga hatua ingawa changamoto ni nyingi.
Afande Sele nzuri_full
Afande Sele

Muziki mwaka 2013 umefanya vizuri. Kama unavyoona wasanii wapya wameibuka na wakafanya vizuri na watu wanaukubali muziki wao. Hata kama ukiangalia matamasha makubwa mwaka huu yaliyofanya vizuri ni ya wasanii wa muziki wa Bongo Flava. Kwahiyo hayo yote ni matunda ya maendeleo ya muziki wa mwaka 2013. Pia mwaka huu kuna wasanii ambao wametutoka,Langa,Omary Omary,Juma Mpogo,pamoja na Mangwea ambaye mwaka huu uwezo wake umezungumziwa sana.Ingawa wasanii wachanga waliofanya poa 2013 wamekuwa wakitunga mashairi mepesi sana ambayo yanaufanya muziki kuwa mwepesi mwepesi,ila tunashukuru Watanzania wameupokea muziki wao na kuusikiliza.
IMG_9733
Young Killer

Kikubwa kabisa ninamshukuru mwezi Mungu kwasababu ndio mwingi wa rehema na amani zipo juu yake. Pili familia yangu ‘Msodoki’ kwa support ambayo inatoka home katika muziki wangu na tatu fans wangu. Mwaka 2013 ndio mwaka ambao umekamilisha 20% ya ndoto za Young Killer kuwa msanii mkubwa katika TV star mkubwa. Kwahiyo mwaka 2013 ni mwaka ambao najivunia kutengeneza fans wengi. Pia nazishukuru media zote zilizonisupport mpaka kufikia hapa nilipo. Tuombe Mungu mwaka 2014 ni mwaka ambao tunajiandaa kwa vitu vipya zaidi.