Blogger Widgets

December 23, 2013

Soma Story Inayozungumziwa Sana Leo Kuhusu Kajala na Mume wa Mtu Ilivyozua Utata

Kajala Masanja.
BAADA ya kuzagaa kwa skandali kuwa mwigizaji Kajala Masanja anatembea na mume wa mtu, staa huyo ameibuka na kueleza kulizwa na ishu hiyo akianika siri nzito ambayo ilikuwa nyuma ya pazia.

Taarifa za awali ambazo Ijumaa Wikienda lilizipata zilieleza kuwa tangu habari hiyo ya mjini ilipuke kama moto wa kifuu kwenye mitandao na baadhi ya magazeti (siyo ya Global), Kajala amekuwa akiishi katika hali ya masikitiko kwani suala hilo limemtesa moyoni.
Kikizungumza na paparazi wetu, chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kilisema kuwa Kajala amekuwa kwenye mateso juu ya skendo hiyo kwani haina ukweli na aliumia zaidi kuona inazidi kubebewa bango kila kukicha na wabaya wake.
“Kajala anazungumza waziwazi kuwa hakuna kitu kinachomtesa kwa sasa kama suala hilo.

 
Kajala.
“Yupo tayari kufunguka ukweli juu ya jambo hilo kwani haoni sababu ya kuumia katika jambo ambalo halina ukweli.
“Kwanza huyo Mwasha (Shamim) anayedaiwa kuwa anaibiwa bwana na Kajala ni marafiki wa kutupwa.
Isitoshe Kajala anafahamiana sana na huyo mume wa Shamim Mwasha (mmiliki wa blogu ya 8020) ambaye ni kigogo mwenye fedha chafu kama yule aliyekuwa akimuwezesha Wema Sepetu,” kilisema chanzo chetu na kusepa.
Akilifungukia Ijumaa Wikienda, Kajala aliamua kupasua jipu kwa kusema kamwe hawezi kutembea na mume wa rafiki yake hata iweje.
Alisema watu wamekuwa wakieneza habari hizo pasipo kuujua undani wa ukaribu wao.
“Nadhani namjua huyu dada siku nyingi sana kabla hata ya wengine kumjua.
“Tunaheshimiana sana na hatujawahi kukoseana sasa sijui nani aliyeanzisha habari ya mimi natembea na mume wake na sijui alifanya hivyo kwa makusudi gani, naumia kila siku kwa ajili ya ujinga wa watu.
“Hakuna ushahidi wowote kuwa natembea na mume wa Shamim, namuomba mpenzi (Shamim) ainjoi ndoa aachane na wapumbavu.” alisema Kajala huku akiangua kilio.