Blogger Widgets

December 30, 2013

Soma Ujumbe wa Martin Kadinda Baada ya Jana Ujumbe Uliosambaa Kutoka kwa Jackcliff Ukisema kama akifa martin Kadinda anajua Chakufanya

Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda anayedaiwa kuwa meneja wa zamani wa Jackie Cliff amesema hajapokea ujumbe wowote kutoka kwa mwanadada huyo anayeshikiliwa kwa tuhuma za madawa ya kulevya huko Macao, China alipokuwa akitokea nchini Thailand.
kadinda
Lisa Jensen, Martin Kadinda na Jackie

Ujumbe ambao ulizaniwa umetumwa na Jack baada ya kupata matatizo.
Ujumbe ulidhaniwa umetumwa na Jackie kwenda kwa Martin baada ya kukamatwa

Martin ameiambia Media kuwa ujumbe uliosambaa katika mitandao, uliandikwa na Jackie mwaka 2010 ambapo alikuwa akimaanisha mambo yaliyokuwa ‘personal’ zaidi.
kc
“Ujumbe uliosambaa ni wa Jackie kweli ila ni wasi kunyingi sana mwaka 2010. Kwahiyo watu walivyoona unafanana na tukio hili wakaona waambatanishe. Nakumbuka ujumbe huu aliuandika sio kwa tukio kama hili yalikuwa ni mambo ya personal,” amesema Martin.
Martin akiwa na Jack

Martin akiwa na Jack

Hata hivyo Martin amesema hawezi kuzungumzia suala la Jackie kukamatwa na dawa za kulevya kwakuwa yeye siyo msemaji.
Jackie Clifford FitzPatrick alikamatwa na madawa ya kulevya Dec 19 mwaka huu akitokea Thailand kwenda Macao alikokamatiwa huku wenzake wawili, Mtanzania na Mnaijeria wakikimbia.