Blogger Widgets

December 17, 2013

Tazama Muoneakano wa Nyumba Iliyoteketezwa na baada ya baba(Mchaga) wa familia hiyo kuhisi kuwa mke wake ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine

Nyumba ya familia moja huko mtaa wa Ugombolwa Kata ya Segerea jijini Dar imeteketezwa kwa moto usiku wa kuamkia jana mara baada ya baba wa familia hiyo kuhisi kuwa mke wake ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine na kuamua kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi.
Segerea, Dar es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa wa Ugombolwa Kata ya Segerea jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Hali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana, ebu ona sasa mwanaume mzima anateketeza nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya shilingi kisa mkewe anatembea nje ya ndoa. Sasa watoto wake wataishi wapi?.. watu wengine ni wajinga sana, kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea shuhuda huyo.

Mpaka mtoa habari hii anaondoka eneo la tukio, nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwa ajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au lah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto