Unaijua Hii Bahati ya Ali Kiba ikiwemo na Kesho kuwa mgeni Rasmi Uswisi
Star wa muziki wa Bongofleva kutoka Tanzania Ali Kiba kesho Ijumaa
tarehe 13/12/2013 atakuwa na show huko Uswisi na mgeni maalum wa show
hiyo atakuwa ni Ashley Toto ambaye ni promota wa wasanii wa Africa
mashariki hususani nchini Ujerumani anakoishi. Ashley pia ni muigizaji
wa filamu za kiswahili katika nchi za Scandinavia akiwa na asili ya
Kenya. Ali Kiba alifanya show Ujerumani wiki iliyopita ambayo
iliandaliwa na Ashley na wenzake nchini Ujerumani na kesho Ali Kiba
atakuwa na show nyingine nchini Uswisi baada ya kuunganishwa na Ashley
na promota wa huko. Akizungumza na Swahilihood Ashley alisema "Show ya German alifanya last Saturday na yuko na nyingine ambayo am the special quest in Swiss, ya Swiss mimi ndio nimemuunganishia na promoter wa huko na hii ya Germany nilikua na wenzangu tuliandaa" Ali Kiba na Ashley Toto