Blogger Widgets

December 12, 2013

Wengi Leo wamesikitishwa na Ni Habari ya Huyu Jamaa aliyepufuliwa macho yake Baada ya kusadikiwa kutembea na mke wa Polisi


Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar, (28) baada ya kupofuka macho.
AMA kweli haki hakuna.


Katika hali ya kusikitisha sana, kijana mmoja Elias John, mkazi wa Kigamboni jijini Dar, (28) amejikuta katika wakati mgumu wa kupofuka baada ya kuchomwa sindano inayodaiwa kuwa na sumu kufuatia kujihusisha kimapenzi na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wa askari Polisi.Akizungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Elias alidai alikumbwa na mkasa huo mwaka 2011 wakati akiwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Amina, ambaye pia alijihusisha na polisi aliyemtaja kwa jina moja la James, aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha Polisi cha Kilwa Road, jijini Dar es Salaam.

“Polisi huyo alikuwa akinifuata mara kwa mara na kuniambia kuwa niachane na mwanamke huyo, lakini kwangu ilikuwa ngumu kwa sababu tulipendana sana,” alisema kijana huyo.

Alisema siku ya tukio, akiwa kijiweni, polisi huyo akiambatana na wenzake, walifika na kumkamata bila kosa lolote na kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi Mianzini, Temeke.

 



Elias John katika pozi akiwa na fimbo yake ya watu wasioona.

Wakiwa kituoni hapo, kijana huyo alisema kwa pamoja Polisi hao walimshika mikono na miguu wakati James alichukua sindano na kumchoma.

Akiwa hajui hatima yake, Elias alisema mara tu baada ya kuchomwa sindano hiyo, alisikia maumivu makali yaliyopanda hadi kichwani na ghafla akapoteza uwezo wake wa kuona.


“Siwezi kuelezea zaidi maumivu niliyoyapata baada ya kuchomwa sindano ile na hapo hapo macho yangu hayakuweza kuona tena licha ya kujitahidi sana,” alisema.
 


Macho ya Elias yalivyoharibiwa na sindano inayodawa kuwa ya sumu.

Alisema baada ya kuchomwa sindano hiyo, askari hao walimtaka aondoke na akajitahidi kuwapa taarifa ndugu zake, ambao walimchukua na kumpeleka Muhimbili ambako hata hivyo walishindwa kumsaidia na hata alipopelekwa CCBRT, pia ilishindikana.

Katika hali ya kusikitisha zaidi, ndugu zake walijaribu kufuatilia suala hilo polisi, lakini walipofika waliambiwa kirahisi kwamba askari hao wote walishafukuzwa kazi.

Alisema juhudi za ndugu zake kuhakikisha haki inatendeka zimegonga mwamba licha ya suala lake kufikishwa kwa taasisi za haki za binadamu ambako bado linashughulikiwa, ingawa hakuna matumaini ya kupatikana kwa ufumbuzi.

“Maisha yangu yamekuwa magumu sana na sijui hatma ya kesi yangu, nitaendelea kuishi hivi mpaka lini? Kwa vile kwa sasa naombaomba tu,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kumuomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuliangalia suala lake kwa undani ili lipatiwe ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment