Blogger Widgets

January 30, 2014

Fid Q, Mrisho Mpoto, Keisha, Bi Chau na King Majuto waigiza filamu iitwayo ‘Pamoko’..Fuatilia Hapa

Fid Q, Mrisho Mpoto, Keisha pamoja na wasanii wa filamu Bi Chau na King Majuto wameunganishwa pamoja na kufanya filamu iitwayo ‘Pamoko’ kwaajili ya kuhamasisha jamii kuhusu walemavu wa ngozi ‘albino’
l
Mrisho Mpoto ameimbia Bongo5 kuwa filamu hiyo ni kwajili ya kuielimisha jamii kuhusu walemavu wa ngozi ‘albino’ na kuonyesha kuwa wana haki sawa kama watu wengine katika jamii.
“Mwaka jana kuna kampuni inaitwa ‘Under the Same Sun’ ilituchukuwa wasanii ambao tunaweza kuwa na ushawishi ili kuielisha jamii kuhusu mauaji ya ndugu zetu walemavu wa ngozi ‘ablino’. Kama unavyojua miaka ya hivi karibuni kulitokea sana mauaji hayo. Kwahiyo sisi tumezunguka katika vijiji vingi sana kuelimisha jamii kuhusu haki na usawa tulionao, bila kujali rangi,kabila wala dini. Kwahiyo tukashoot vipande kama series ambavyo vinaweza kuonyeshwa na kuelimisha jamii,” amesema Mrisho.

“Mimi sio msemaji mkuu , Under the Same Sun’ ndo ilisimamia shughuli zote hizi,kwahiyo filamu najua itatoka hivi karibuni. Kwahiyo filamu hipo ni ya kuelimisha jamii kuhusu masuala ya albino,utamuona Fid Q, Mrisho Mpoto, Keisha, Bi Chau na King Majuto.”
from:bongo5