Blogger Widgets

January 6, 2014

Maneno Mazito ya Zito Kabwe Kwenda kwa Tundu Lissu

Mbowe, Zitto na Lissu mstari wambele enzi hizooooo

 

"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma vijijini. Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa Mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa. Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative party?
 

Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda.
Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya Umma ilipo Club Bilicanas.

They must know I am not a push over. Chacha died, I won't.
Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."

wapenzi jana nilikuwa nimetulia zangu nyumbani , ghafla jioni kwenye twitter nikaona taarifa kuwa Mheshimiwa alipewa magari mawili sijui na nani.
 Zitto akaweka hiyo status facebook, heeeee chinekee siri nzito nzito zimeanza kuwekwa hadharani atiii, Kelele nyingiiii kumbe kuna mipango underground. 


Bei ya umeme imepaa ile mbaya lakini wanasiasa wapojeeee busy kutoleana ya ndani mara Kifaranga Heeeee jogoo nani sasaaaa?

chinekeeee siasa zinalipajeeeeee mpaka Tsh 200M watu wanavuta. Lolest. Waache wachambane sie tuujue ukweli Lol

hebu nivute kiti zaidi na niagize popcorn kwaajili ya kujionea maajabu ila kuna mwanasiasa hapo ananishangaza yaani hawataki kukubali kushindwa ukisema yaishe uta'ngatwa.. haya mambo ya kutoleana siri ktk social media sie tunawachora jinsi mlivyokuwa ila we wont help, kwanini msikae mkayamaliza huko... ila jueni magazeti, blogs, twitter, fb hazitowasaidia kaeni chini m discuss wenyewe mnajitia aibu....