Blogger Widgets

January 28, 2014

Picha za Kusisimua za Mtoto aliyekumbwa na Gonjwa la Ajabu


 Honolina akijitahidi kufukuza nzi waliojazana kwenye vidonda vyake
 Kutokana na ugonjwa huo wa ajabu macho ya mtoto huyo yamekufa
 Nyama la pili mfano wa pembe lililoota mgongoni

 Bi,Grece John mama mzazi wa mtoto huyo ambaye amekubali kukatwa makalio yake ili mwanaye apone
 Honalina akinywa maji baada ya kupigwa na jua kali alipokuwa akiomba sendi ya mabasi msamvu Morogoro wiki iliyopita
 Mpiga debe huyo baada ya kumuona live mtoto huyo alishindwa kujizuia na kumwaga machopzi hadharani

    Wananchi wakimchangia mama huyo
 Honolina mbaye ugonjwa huo umeababisha miguu yake kuishiwa nguvu na kushindwa kusimama
 Mwandishi wa habari hizi ambaye anaifuatilia kwa karibu famili hiyo mwaka Mach 17 2012 alifika wodi namba 4 hospital ya mkoa wa Morogoro na kumkuta mama huyo akiwa amelazwa na mtoto wake huyo ambaye wakti huo manya makubwa yalikuwa bado hayajaanza kumtoka kama anavyooneka pichani,aliyepakatwa na mtoto wa mwisho wa mama huyo.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
LAZIMA utokwe machozi! Grace John mkazi wa Mzumbe, Mvomero mkoani Morogoro yupo kwenye wakati mgumu kutokana na maradhi ya ajabu yanayomsumbua mwanaye Honolina Christian Mkude (11).
Honolina anasumbuliwa na ugonjwa wa kuota nyama sehemu za mwili wake zinazofanana na pembe za mnyama, ugonjwa ambao unamtesa tangu kuzaliwa kwake.
ILIKUWAJE?
Akisimulia kisa kizima, mama mzazi wa Honolina, Bi. Grace, anasema tangu amemzaa mwanaye huyo ni mitihani baada ya mitihani.
Mazungumzo hayo yalifanyika hivi karibuni katika kituo cha mabasi ya mikoani, Msamvu, mjini hapa wakati mama huyo na mwanaye wakihangaikia kuchangisha fedha za usafiri wa kwenda Moshi kutafuta tiba zaidi katika Hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC).
“Ndugu mwandishi, kwa kweli sijui hatima ya mwanangu. Nilimzaa akiwa ameota nywele sehemu zote za mwili wake, hadi usoni. Mimi na mume wangu tulishangaa, lakini tuliendelea na matibabu katika hospitali mbalimbali maana baadaye alianza kupatwa na uvimbe.
MTIHANI MWINGINE
“Jamani ndugu yangu... Mungu ana mitihani yake. Mume wangu (Christian Mkude) ambaye ndiye alikuwa tegemeo pekee kwetu, alifariki mwaka 2007 kwa ajali ya gari, wakati akisaka fedha za  matibabu ya mwanetu.
“Kifo chake, kwangu kimekuwa pigo mujalabu. Sina pa kukimbilia na hivi juzi tu tulikuwa tumelazwa Hospitali ya Mkoa (Morogoro) na hapo tumepewa barua ya kwenda KCMC kwa matibabu zaidi.
“Hivi unavyoniona nachangisha fedha ili nipate angalau nauli za kutufikisha kwanza hospitalini.  Nimechanganyikiwa kabisa,” alisema Bi. Grace kwa majonzi na kuongeza:
“Wakati tatizo la mwanangu linaanza sikutegemea kama siku moja angekuja kuwa hivi. Zilianza kuota nywele mwili mzima, baadaye vidonda vikaanza kumtoka na sasa hali imebadilika na kuota nyama hizi kubwa kama mapembe kama unavyoona.”
SAUTI YA BI. GRACE KUTOKA MOSHI
  Juzi mwandishi wa habari hizi ambaye anaendelea kuifuatilia familia hiyo alimpigia simu Bi,Grece kwalengo la kujua kama  wamefika salama,"Mungu akubariki sana kwa kutupigania tunamshukuru mungu tumefika salama,Misaada ya fedha kidogo tuliopata pele stenzi za daladala na ile ya Msamvu kutoka  kwa wasamaria wema Msamvu, ilitusaidi kusafiri hadi Moshi na kufika katika Hospitali ya KCMC''alisema mama huyo.

BADO ANAHITAJI MSAADA
“Madaktari wametupa moyo, wamesema watajaribu kumsaidia mwanangu. Watamtoa hizo nyama ila kwa sababu kutabaki na mashimo lazima wapandikize nyama nyingine.
“Tumeshakubaliana kuwa mimi ndiye nitakayekatwa sehemu ya nyama kutoka kwenye makalio yangu kwa ajili ya kumsaidia mwanangu,” alisema Bi. Grace, kilio kikisikika kwenye simu.

Akaongeza: “Wameshachukua nyama za mwanangu na kwenda kupima na baadaye watachukua zangu ili kuona kama zinaendana, upasuaji ufanyike. Gharama kwa ajili ya matibabu hayo wamesema ni shilingi 400,000 na mimi sina uwezo.
“Watanzania wenzangu, naombeni mnisaidie ili niweze kuondokana na hili tatizo. Mimi ni mjane na sina kazi ya kueleweka, napigania uhai wa mwanangu. Naombeni msaada wenu,” alisema.

Akaongeza: “Wameshachukua nyama za mwanangu na kwenda kupima na baadaye watachukua zangu ili kuona kama zinaendana, upasuaji ufanyike. Gharama kwa ajili ya matibabu hayo wamesema ni shilingi 400,000 na mimi sina uwezo.
“Watanzania wenzangu, naombeni mnisaidie ili niweze kuondokana na hili tatizo. Mimi ni mjane na sina kazi ya kueleweka, napigania uhai wa mwanangu. Naombeni msaada wenu,” alisema. 
SHIRIKI BARAKA
Kumsaidia mhitaji wa kweli huongeza baraka katika kipato, vitabu vitakatifu vinaeleza wazi. Ndugu wasomaji wetu wapenzi, kwa yeyote atakayeguswa na mateso ya familia hii, anaweza kumsaidia chochote mama huyo kupitia simu zake namba 0719 749542 (Tigopesa) na 0762 425973 (M - pesa).