Blogger Widgets

January 28, 2014

Soma Mambo Yanayomsibu Msanii PNC Baada ya Kujiondoa kundi la TipTop Na Kwenda Kwa Ostaz Juma na Musoma

Msanii wa muziki nchini, Pancras Ndaki maarufu PNC amesema mpaka sasa haelewi anaenda wapi na muziki wake baada uongozi unaomsimamia ‘Mtanashati Entertainment’ kutotambua kama upo naye pamoja ama tayari amepigwa chini.
Wasanii wa Mtanashati Entertainment kushoto ni Happy Balice , Dogo Janja na Pnc
Wasanii wa Mtanashati Entertainment kushoto ni Happy Balice,Pnc na Dogo Janja

Akizungumza na Bongo5 leo, PNC amesema amekuwa akijitahidi kufanya nyimbo nzuri lakini anashindwa kufika popote kutokana na uongozi wake kutokuwa makini na msanii huyo.
“Ulimwengu wa muziki upo simple sana,mimi muziki najua kuimba na mashabiki wangu wanajua mimi naweza muziki,tatizo kitu kimoja kinachonifelisha mimi ni uongozi nilionao haueleweki,kama ningepata uongozi ambao unafuatilia muziki na unaujua muziki ningekuwa mbali sana.Uongozi wa Ostaz Juma siuelewi elewi kabisa, sijui kuna vitu vimemkatisha tamaa,hata sielewi muziki wangu unaenda wapi? Yaani nashindwa kuelewa kabisa,Ostaz yuko busy yaani hata sijielewi kama nipo na Ostaz ama vipi,” amesema msanii huyo.

“Leo nimeanza kumtafuta nimemtumia meseji, nataka nitambue kama tuko pamoja ama mimi niendelee na kazi zangu. Mimi nadhani muda wangu umefika wa kuamka. Watu wamekuwa wakiniuliza kwani bado upo kwa Ostaz? Yaani wananiona sieleweki,kwahiyo namtafuta nikimpata nikae naye chini niongee naye nijue kimoja kinachoendelea ni nini. Sishindwi kutunga nyimbo nzuri za kuwavutia watu. Nyimbo ngapi nzuri zimeshindwa kusimamiwa? Watu wanajua PNC anaweza fanya muziki mzuri,inauma sana kwanza sikupenda masuala haya kuyazungumzia kwenye Media ila imenibidi kwasababu watu wanataka kujua,” amesema PNC kwa uchungu.