Blogger Widgets

January 30, 2014

Soma Maswaibu Yaliyomkuta Msanii Dude

HALI ya uchumi ya mwigizaji Kulwa Kikumba ‘Dude’ imemkwamisha mwigizaji huyo ashindwe kurekodi tamthiliya yake.
 
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Akizungumza na paparazi wetu, Dude alikiri kuwa uchumi umemkalia vibaya ambapo aliruhusiwa kupewa muda wa hewani katika Runinga ya East Africa lakini akashindwa kushuti kutokana na majukumu ya kifamilia kumuandama.
“Daa we acha tu, mwezi wa kwanza huu majanga matupu. Nimeshindwa, kama unavyojua nina watoto wengi mambo ya ada yamenibana kwelikweli,” alisema Dude ambaye ana jumla ya watoto sita kwa mama tofauti.