Tunaomba radhi kwa hizi picha kwa yeyote zitakayemkera..!
HUWA YANASIKIKA KUTOKEA LAKINI LEO NI LAIVU BILA CHENGA…… Mahabusu mmoja
aliyekuwa mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya
Mwanzo iliyopo eneo la jirani na Mamlaka ya maji safi na Hifadhi ya
Mazingira (MWAUWASA) jijini Mwanza alitoa vioja vya mwaka kwa kujaribu
kutoroka kwa kujipaka kinyesi ili asiguswe wala kukamatwa.
Askari
akiwa amemnasa mahabusu aliye kimbia mara baada ya kujipaka kinyesi
katika mahabusu ya mahakama ya wilaya ya Nyamagana na Mahakama ya
Mwanza.
Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake halikufahamika alijimwagia kinyesi
kilichokuwa kwenye ndoo iliyokuwa ndani ya sero ya Mahakamani hapo na
askari alipokwenda kufungua ili kuwapeleka watuhumiwa kwenye chumba cha
Mahakama kusomewa kesi yake baada ya kutajwa na karani wa Mahakama ya
mwanzo, baada ya kutajwa ndipo mahabusu huyo alipopata mwanya wa
kukimbia na kutoa tahadhari kwa atakaye mgusa au kumshika atakumbana na
kadhia ya kuchafuliwa kwa kupakwa kinyesi.
Askari mwingine mwenye cheo cha sajenti, ambaye alikuwa
akihushughulika na huduma nyingine mahakamani hapo, kwa kuwa alikuwa na
uzoefu wa kupambana na mikasa na vioja kama hivyo vya mahabusu wanao
kula njama za kutaka kutoroka aliamua kula naye sahani moja kwa
kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata.
Baada ya kumkamata na kumrejesha katika chumba cha mahabusu mahakamani
hapo, kwanza mtuhumiwa huyo aliamriwa kuzoa mtondoro wa kinyesi cha
binadamu alichokuwa amejimwagia na kutapakaa chini na mara baada ya
kumaliza kuzoa uchafu huo, alipelekwa kwa hakimu ambapo alisomewa kosa
la kula njama za kutoroka na kukumbana na adhabu nyingine ya kuhukumiwa
kifungo cha miezi sita (6) jela, huku kesi yake iliyokuwa ikimkabili
awali ikiahirishwa.
“Kama alivyojipaka ndivyo alivyo yazoa…”
Moja baada ya jingine.
Hatua kwa hatua chini ya ulinzi mkali wa askari shupavu.
Huku
akiweka kinyesi hicho kwenye ndoo mahabusu huyo alilazimika kukizoa kwa
mikono kama muuza mkaa apimavyo mkaa kwenye kopo kuwauzia wateja wake.
Mchafuzi wa mazingira akiadabishwa kabla ya kwenda kusomewa kesi nyingine ya kula njama za kutaka kutoroka.
CREDIT : G SENGO MWANZA & Bongoclantz
No comments:
Post a Comment