Blogger Widgets

February 3, 2014

Baadhi Ya Picha za Tukio Lililokuwa Linazungumziwa Toka Jana Jinsi Jokate Kidoti alivyowafanyia Surprise Wema,Kajala na Aunt Eze Kwenye Show ya Arusha

IMG-20140202-WA0012
Unaweza kujikuta ukishindwa kuielewa hii hali lakini inabidi ukubaliane na ukweli halisi wa hiki kilichotokea,Jokate na Wema historia yao ilianzia kwenye shindano la kumtafuta Miss Tanzania 2006 ambapo Mshindi alikua ni Wema Sepetu akifatiwa na Jokate kisha mshindi wa tatu akiwa Lissa Jensen.

2006
Headline zilikuja kutengenezwa tena zikiwahusisha warembo hawa kuonekana wako na mtu mmoja ambapo magazeti mengi yaliandika mahusiano haya  yaliyokua yakimhusu Diamond Platnumz kutoka na warembo hawa.

IMG-20140202-WA0009
Kimepita kimya kirefu sana juu ya hawa watu wawili hadi usiku wa February 01 huko Arusha kwenye Tamasha la Divaz Night Endless Fame ambalo ndani yake kulikua na mastar kadhaa akiwemo Wema Sepetu,Aunt Ezekiel,Martin Kadinda,Kajala,Zamaradi Mketema,Chid Benzi,Mirror,Jordan na wengine kibao.
IMG-20140202-WA0011
  Wakati Madam Wema Sepetu akimwaga mauno kwenye jukwaa bila kutegemewa na mtu yoyote Jokate alipanda Jukwaani na kuanza kumtunza Wema pesa na wakati huo Wema alikua akicheza Wimbo wa Diamond My Number One ‘Ngololo’ ambapo Jokate aliungana na Wema kuucheza Wimbo huo.
http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/02/IMG-20140202-WA0008.jpg


 
Kajala, Wema, Aunt na Zamaradi wakiwa katika pozi tofauti.


....Wakiwa pamoja na Mirror tayari kwa ajili ya kwenda kwenye Show, klabu ya  Triple A.


Wema Sepetu, Aunt Ezekiel na Kajala Masanja tayari kwa ajili ya kwenda ukumbini.

Kajala akipanda stejini.

Wema akipanda jukwaani huku akiacheza.

...Wakiwa katika picha ya pamoja.
..
.Wakicheza na Mirror.

Wema katika pozi.

Msanii Dyana Kimaro katika pozi.

Wema Sepetu pamoja na Meneja wake Martin Kadinda muda mfupi baada ya kuwasili jijini Arusha.

  Wema Sepetu, Zamaradi na Martin Kadinda katika picha ya pozi.