Blogger Widgets

February 4, 2014

Kwa Hili Young D Anahitaji Pongezi

Wakati ambapo rappers wengi wa Tanzania wanalalamika kuwa muziki hauwalipi kivile kutokana na kazi kubwa wanayofanya, kuna baadhi ya rappers ambao wana mtazamo tofauti na kwao rap ya Tanzania imewawezesha kufanya vitu vikubwa kuanzia katika ngazi ya familia, na wanaushukuru muziki wa Tanzania kwa hatua hiyo.
Rapper mwenye uwezo mkubwa wa kurap kwa Kiswahili fasaha, Young Dee, ni mmoja kati ya rappers ambao kwao muziki umewatendea haki na hawaoni haja ya kulalamika.
Akiongea na tovuti ya Times Fm, Young Dee amesema anauheshimu sana muziki wa Tanzania kwa kuwa umeweza kusaidia kuirudisha heshima ya familia yake baada ya kuweza kutumia kipato anachokipata kwenye muziki kuikomboa nyumba ya familia yao iliyotakiwa kuuzwa ili kufidia deni la marehemu baba yake la kiasi cha shilingi million 37 .
“Marehemu baba yangu alikuwa ana deni kubwa ambalo hakuna mtu ambaye alikuwa anaweza kuilipa hilo, kwa hiyo ilikuwa ni nyumba ambayo iliikuwa imekaa imetelekezwa na imeharibika japo ilikuwa imejengwa kwa mfumo wa kisasa kidogo lakini bado inahitaji kuongezewa nguvu. Young Dee ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Kwa hiyo niliweza kutumia pesa yangu kuclear hilo deni na kuweza kuiregister upya kama nyumba yangu sasa. Kwa sababu ilikuwa na madeni na ilikuwa iuzwe kwa thamani ya million 37. Kwa hiyo hilo deni limeweza kuli-clear, kwa hiyo hicho ni kikubwa zaidi kwa hiyo sasa hivi iko pale inanisubiri mimi nikusanye tena nguvu nimalizie mambo machache niweze kuhamia.” Ameongeza.
Amesema kwa kuzingatia hilo, mama yake ameweza kuwa na furaha zaidi na muziki anaoufanya hata kuliko yeye mwenyewe (Young Dee). Ameongeza kuwa kuwa kwa muda mrefu yeye amekuwa akiishi katika nyumba za kupanga lakini kufikia mwezi wa nane atakuwa amemaliza kuikarabati nyumba hiyo na kuhamia.
“Kufikia mwezi wa nane naweza kumpigia simu mama yangu na kumwambia, mama njoo ukae kwangu.”
Kwa upande mwingine, Young Dee amesema video ya Kijukuu ilimlipa zaidi ya gharama alizotumia kuifanya na kwamba ana mpango wa kufanya video nyingine kali ya wimbo wake ‘Fununu’ aliofanya na mwana FA na kwamba ana ma-director wawili kichwani kwake akiwemo Nisher aliyefanya video ya ‘Kijukuu’