Blogger Widgets

February 26, 2014

Soma Alichozungumza Kajala baada ya kuishwa kitu chenye Sumu Ndani yake

Muigizaji wa filamu, Kajala Masanja amesema afya yake bado haijakaa vizuri baada ya kunywa kitu chenye sumu kwenye show ya Izzo Bizness iliyofanyika Club 71, Tegeta Kibaoni Jumapili iliyopita.
Kajala Masanja akiwa katika pozi
Kajala Masanja akiwa katika pozi

“Naendelea hivyo hivyo,” Kajala anayeongea kwa shida ameiambia Bongo5. “Nilivyoenda kwenye show nimefika nikawa nakunywa ghafla nikaanza kujisikia vibaya nikawaambia wanipeleke nyumbani. Ghalfa nikaanza kujitapikia,kujitapikia mpaka nikafika nyumbani nikapelekwa hospitali nilivyopimwa wakasema nimekula kitu kibaya.”

Kajala amesema hakumbuki kama alikula kitu kingine zaidi ya glasi moja na Cocktail. Show ya Izzo ilisindikizwa na wasanii kibao wakiwemo Vee Money, Gosby, Snura Mushi, Shetta, Barnaba Boy, Jux na wengine.