Blogger Widgets

February 13, 2014

Soma Dili alilopewa yule kahaba ambae ni Albino aliyematwa mara kadhaa Huko Morogoro Akijiuza



                           




 Mwenyekiti wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisni kwake
 Lakia Mussa Kulia] mhasibu mkuu wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro aki copy picha za Fidhira
Fadhira kushoto mama wa watoto wa watatu akihojiwa na mwenyekiti wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro David Mganga

Akiwa mbele ya uongozi mzima wa chama cha Albino mkoa wa Morogoro akitakiwa kutoa maelezo kwani alikamatwa na baadae kutolewa kwenye magazeti akifanya biashara ya kujiuza,jambon ambalo limewadhalilisha maalbino wenzake


BAADA ya kunaswa na kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu'OFM' kilichopo chini ya kampuni ya Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi,Ijumaa,Risasi Aman na ljumaawikienda Changudoa Albino Fadhira Omari wakati wowote kuanza sasa atafunguliwa duka kubwa na chama cha Albino Tanzania

Hatua hiyo imekuja baada ya Uongozi wa Juu vya chama cha Albino Mkoa wa Morogoro kusoma moja ya magazeti ya Global Publishers yalioripiti habari za Albino huyo kunaswa  kambi ya machangudao ya Khahumba mkoani hapa usiku wa manane akiuza mwili wake kwa bei ya shilingi elfu 7 kila kichwa.

Baada ya kusoma gazeti hilo mwenyekiti wa chama cha Maalbino mkoa wa Morogoro Bw David Mganga alisaka namba ya simu za Mwandishi wa habari hizi na kumwita ofisi za chama cha maalbino mkoa wa Morogoro, ambapo pamoja na mambo mengine alikipongeza kikosi kazi cha OFM kwa kufanya kazi nzuri ya kufichua maovu.

" Nakupongeza sana kwa kazi nzuri mliofanya ya kukamata Albino akijiuza nimekuita unisaidie mambo mawili moja naomba picha zote za tukio lile na pili naomba unisaidi kumpata yule Albino mliomnasa"alisema mwenyekiti huyo.

Mwandishi wa OFM alitekeleza maombi hayo  ambapo siku iliyofuata uongozi mzima wa chama cha Albinoa mkoa wa Morogoro ambao pia ulimwalika mwandishi wa Global Publishers  ulimuweka mtu kati Fadhira ambaye kwenye maelezo yake alidai anafanya kazi hiyo baada ya kutelekezwa na mumewe aliyeza naye watoto watatu ambao wote  hawana ulemavu huo wa ngozi.

Uongozi huo wa mkoa ulipanga kumsomesha na baadae kumtafutia kazi kwa kushirikiana na serikari Fadhira alikata ofa hiyo akidai kwamba ana matatizo ya macho hivyo hatoweka kusoma na aliomba gharama hizo za masomo zitumike kumfungulia duka jambo ambalo uongozi huo ulikubali kwa mashariti ya Fadhira kutofanya tena biashara hiyo ya kuuza mwili wake.

Baada ya makubaliano hayo uongozi huo uliwasiliana na uongozi wa chama cha Albino taifa kwa utekelezaji wa kumfungulia duka Fadhira

No comments:

Post a Comment