Blogger Widgets

February 19, 2014

Soma Jinsi Juma Nature alivyojitetea Kuhusu Kumdiss Diamond Kwenye Ngoma yake kwa Kumita dada Mondi

Hatimaye Juma Nature, amezungumzia utata ulioibuka kwenye wimbo wake mpya Kama Jana, unaohusiana na kama kweli amemdiss Diamond.
Akiongea na kipindi cha Showtime Next Chapter, Juma Nature aka Kiroboto amesema jina la ‘Dada Mondi’ lililofanya wengi waamini kuwa ni version yake ya Diamond, ni jina la msanii mwingine kabisa. “Hamna diss ya kumdiss Diamond, Diamond hajadisiwa,” amesema Nature. “Pale katajwa mtu mwingine kabisa anaitwa Dada Mondi

na anakaa mitaa ya kwetu. Bado hajatoka halafu anataka sifa.”