Blogger Widgets

February 6, 2014

Soma Kisa cha PNC Kufukuzwa na Ostaz Juma na Musoma kwenye Kundi la Watanashati

Msanii aliyekuwa chini ya kampuni ya Mtanashati Entertainment, Pancras Ndaki aka PNC amesema ameamua kuachana na kampuni ya hiyo na kujiunga na Top Fleva,akidai bosi wake wa zamani amekuwa akimsema vibaya na kumchafua kwenye jamii.
Wasanii wa Mtanashati Entertainment kushoto ni Happy Balice , Dogo Janja na Pnc
Akizungumza na Bongo5, PNC amesema haoni sababu ya kuendelea kukaa na kampuni ambayo haiendelezi muziki wake, bali ni kuchafuana kwa jamii.
“Mimi hajanilipia hoteli zaidi ya kunilipia kodi ya nyumba ya mwaka. Hayo mambo ya hoteli sijui yametoka wapi?,anasema hivyo ili nionekane mtu mbaya. Kwahiyo mimi nimeamua kuondoka kwenye usimamizi wake. Kwa anakuwa mwingi wa ahadi kuliko kutekeleza na kwenye media anatusemea vibaya. Mimi nimeshajiunga na Top Fleva na tumeanza kurekodi kazi mpya,” amesema.

Boss wa Mtanashati, Ostaz Juma jana aliiambia tovuti ya Times FM kuwa PNC na Dogo Janja hawana nidhamu na kwamba pesa alizokuwa anawekeza kwa wasanii hao ni bora akatoe sadaka.
“Sio yeye tu, na Dogo Janja, wote hawana utovu wa nidhamu kabisa, mara kumi fedha zangu nizipeleke msikitini au kwa watoto yatima nibarikiwe kuliko kukaa na watu wasiokuwa na nidhamu,” alisema.