Blogger Widgets

February 26, 2014

Soma Mnaneno haya ya Huyu Msanii wa Kike wa Bongo Movie aliyekamatwa siku chache akiwa anajiuza Live na Kukubali ni kweli LAKINI..?

SIKU chache baada ya msanii anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ kuingia kwenye kumi na nane za mtego wa kujiuza wa kikosi kazi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, ameibuka na kusema, anajuta, amekoma na hatarudia tena.


Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika ofisi za GPL akiongea na OFM.
Habari ya Vai kunaswa katika mtego wa kujiuza iliripotiwa na gazeti damu moja na hili, Ijumaa toleo la wiki iliyopita, ambapo msanii huyo aliingia mkenge baada ya kukubali kukutana na ‘pedeshee’ mmoja kutoka mkoani kwa lengo la kumpa uroda kwa malipo ya shilingi 500,000.

Vai alivyonaswa akiwa mawindoni.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko juzi, Jumatatu jijini Dar es Salaam, Vai alisema: “Kiukweli lile tukio lilinichanganya sana lakini pia limenipa fundisho kubwa. Nawaomba ndugu zangu na mashabiki wangu wote wanisamehe kwa dhati kabisa.

Vai akificha sura yake baada ya kunaswa na OFM.
“Naahidi sitarudia tena ujinga kama ule. Ilikuwa ni tamaa tu. Hivi ninavyozungumza na wewe nipo kwa editor (mhariri) nasimamia editing (uhariri) ya filamu yangu ambayo ipo katika hatua za mwisho kuingia mitaani. Niko bize na kazi, acha niwekeze kwenye ujasiriamali tu. Nawashauri wasanii wenzangu tutulie maana OFM wapo macho.”

...Akimsubiri pedeshee.
Alisema, katika filamu yake hiyo aliyoipa jina la Beautiful Liar amewashirikisha wakongwe Mohammed Fungafunga ‘Jengua’, Hashim Kambi ‘Wingo’ na mastaa wengine kwenye tasnia hiyo na kwamba mashabiki wake wakae mkao wa kula.

...Baada ya mchezo kuharibika.

No comments:

Post a Comment