Blogger Widgets

February 6, 2014

Tazama na Soma Mambo yanayoendelea Kati ya Wema Sepetu na Naima wa Clement..

Msanii wa filamu na CEO wa Endless Fame Films, Wema Sepetu amesema hawezi kuumizwa na kitendo cha rafiki yake Naima Shaa aliyemchukulia mpenzi wake Clement Kiondo na kumtaka mwanadada huyo aendelee na maisha yake.
Akizungumza na U Heard ya Clouds FM,Wema amesema maisha yake ya furaha yanaendelea kama kawaida kwasasabu haangalii nyuma.
“I don’t want to talk about it,” amesema Wema. “Kwasababu hata siangalii nyuma you know maisha yameendelea am happy, that thing I want ni mimi kuwa happy,kwasababu nisingekuwa happy ningekuwa nasema labda Naima ananiumiza,lakini hawezi kuniumiza nimeshamwambia mpaka Naima. Nimemwambia ‘ishi maisha yako,fanya mambo yako’, mbona tunaongea tu na Naima fresh wala Naima na huyo mtu, yani they can do anything sitamind.”
69afe9be7f7511e3b8e31277082b5ce5_8
Naima
“Huyo mtu yupo na mtu wake,mimi nyenyewe si nipo na mtu wangu, kila mtu kashafanya mambo yake basi.”
Katika hatua nyingine, Wema amekanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii wa kampuni yake, Mirror.
“I can never do something like that,ukisema hivyo unanidisrespect mimi,” alisema.