Blogger Widgets

February 28, 2014

Tazama Pica za Wasani wa waliozindua kampeni ya kitaifa kuishinikiza serikali kuwatambua katika katiba


Leo asubuhi  (February 28) pande za Kinondoni Vijana Social Hall kulikua wasanii wa fani mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kitaifa maalum kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuwatambua wasanii kikatiba.
Licha ya kuwa na shinikizo hilo lakini pia kutakuwa na  maandamano ya amani wanayotarajia kuyafanya ikiwa ni sambamba na kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kumteua mmoja wao (hajafahamika bado) washiriki kuhudhuria katika bunge la katiba.
tumepiga na nikki wa pili moja kati wasanii waliopo mstari wa mbele kwenye movement hii"Tumezindua kampeni yetu ya kitaifa kushinikiza serikali itambue wasanii kama kundi maalum kwenye jamii na kuingizwa kwa haki bunifu katika katiba hizo ndio hoja zetu mbili tunazozipigia kelele" amesema Nikki wa Pili 
lakini pia ameendelea kusema "Tutafanya maandamano na kumfahamisha Raisi Jakaya Kikwete kuwa sekta ya ubunifu inaingiza mapato kuliko sekta ya Nishati na Madini ambayo inajadiliwa kila siku bungeni, lakini sekta ya ubunifu imesahaulika"