Blogger Widgets

February 26, 2014

Tazama Picha jinsi PNC alivympigia magoti Ostaz Juma ILI aArudishwe tena kwenye kundi la watanashati Baada ya kujitoa.Hii ni mfano wa jinsi wasanii wengi wanavyodhalilishwa.

Wakati mwingine matatizo na shida kwenye maisha hutufanya tufanye maamuzi magumu yanayoweza kutudhalilisha mno kwa watu wanaotufahamu. Kila mtu ana shida zake na Mungu kampa kila mmoja roho yake tofauti ya kuweza kustahili dhoruba katika maisha.
2
PNC akipiga magoti kumuomba Ostaz Juma amrudishe Mtanashati Entertainment

Malalamiko kuhusu muziki wa Tanzania kuwa mgumu, yamekuwa kama wimbo unaosikika kila siku kwenye masikio ya watu na ni kweli lisemwalo lipo. Wasanii wengi wana siri zao moyoni lakini hali halisi ni kuwa, wengi wanaishi maisha magumu.
Kwa muda mrefu, muziki wa PNC aliyekuwa akisimamiwa na kampuni ya Mtanashati Entertainment ya Ostaz Juma umekuwa ukienda mrama. Amekuwa akijaribu kutoa nyimbo za kila aina kujaribu kulishawishi soko gumu la muziki wa Bongo, lakini mambo yameendelea kuwa magumu upande wake. Hali hiyo ilimfanya achukue uamuzi mgumu wa kujiondoa na kwenye kampuni hiyo, kwa madai kuwa haoni chochote cha maana anachokipata na ni kama vile bosi wao amewatelekeza.
“Ulimwengu wa muziki upo simple sana,mimi muziki najua kuimba na mashabiki wangu wanajua mimi naweza muziki,tatizo kitu kimoja kinachonifelisha mimi ni uongozi nilionao haueleweki,kama ningepata uongozi ambao unafuatilia muziki na unaujua muziki ningekuwa mbali sana.Uongozi wa Ostaz Juma siuelewi elewi kabisa, sijui kuna vitu vimemkatisha tamaa,hata sielewi muziki wangu unaenda wapi? Yaani nashindwa kuelewa kabisa,Ostaz yuko busy yaani hata sijielewi kama nipo na Ostaz ama vipi,” PNC aliiambia Bongo5 siku chache kabla ya kutangaza kujiondoa Mtanashati.
“Leo nimeanza kumtafuta nimemtumia meseji, nataka nitambue kama tuko pamoja ama mimi niendelee na kazi zangu. Mimi nadhani muda wangu umefika wa kuamka. Watu wamekuwa wakiniuliza kwani bado upo kwa Ostaz? Yaani wananiona sieleweki,kwahiyo namtafuta nikimpata nikae naye chini niongee naye nijue kimoja kinachoendelea ni nini. Sishindwi kutunga nyimbo nzuri za kuwavutia watu. Nyimbo ngapi nzuri zimeshindwa kusimamiwa? Watu wanajua PNC anaweza fanya muziki mzuri,inauma sana kwanza sikupenda masuala haya kuyazungumzia kwenye Media ila imenibidi kwasababu watu wanataka kujua,” alisema PNC kwa uchungu.
Haikuchukua muda, PNC alitangaza kujiondoa kwenye kampuni hiyo.
“Nimeamua kuondoka kwenye usimamizi wake. Kwa anakuwa mwingi wa ahadi kuliko kutekeleza na kwenye media anatusemea vibaya. Mimi nimeshajiunga na Top Fleva na tumeanza kurekodi kazi mpya,” PNC aliiambia Bongo5.
Muda si mrefu, uamuzi aliouchukua PNC umeanza kuonekana kama kuruka majivu na kwenda kukanyaga mkaa wa moto na sasa anahisi ni bora arudi kwenye majivu anayoweza kuyavumilia. PNC amerudi kwa bosi wa zamani kumpigia magoti na kumuomba amrejeshe kwenye himaya yake.
Huo ni ushindi kwa Ostaz Juma. Inaweza kuonekana kama movie, drama ama publicity stunt kwakuwa ndo mchezo wa siku hizi, lakini si jambo la kuchukua muda kuamini kwakuwa ni kweli hali ya PNC kimaisha ni mbaya.
3

Kuna tetesi kuwa maisha kwa msanii huyo yamekuwa magumu kiasi ambacho ameshindwa hata kulipia kodi ya chumba anachoishi.. Ni jambo la kusikitisha kusikia linamtokea msanii mwenye jina na uwezo kama PNC, lakini hiyo ndio hali halisi ya muziki wa Bongo Flava, wanaofaidi ni wachache. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa, ni Ostaz Juma mwenyewe ndiye anayemchoresha PNC kwa kuweka video na picha zinazomuonesha PNC akimpigia magoti kumuomba msamaha. “Jamani muziki ni mgumu sana, PNC karudi kwa kuomba msamaha kwa boss wake Ostaz juma,” ameandika Ostaz kwenye ukurasa wake wa Facebook kwenye video hiyo.
Kama hili ni tukio halisi na si la kutengeneza, PNC amechukua uamuzi mgumu ambao kwa wenye roho za kijerumani kufa na tai shingoni, wasingeweza kufanya.
Huu ni mfano tu wa jinsi ambavyo maji ya shingo yamewafika wasanii wengi na kwakuwa hawana jinsi, huamua kuweka sifa pembeni na kuwatukuza wale wanaohisi wanaweza kuwasaidia. PNC anahitaji kusaidiwa na kuoneshwa njia na mtu ambaye hatokuwa na matarajio ya haraka ya kumuingizia faida. Anahitaji kukalishwa chini na kupewa elimu na muelekeo mpya wa muziki wake. Lasivyo, hata kama atarejea tena kwenye kampuni hiyo, hatoweza kwenda popote zaidi ya kusaidiwa tu fedha za kujikimu na kulipa kodi za nyumba, vitu ambavyo haviwezi kudumu na Ostaz atachoka tena.
From:Bongo5