Blogger Widgets

February 22, 2014

Tazama Picha ya Mchumba wa Miss Tanzania Hii Na Baada ya Kusmbuliwa Sana

MISS Tanzania mwaka 2011, Salha Israel amevunja ukimya baada ya kumuweka wazi mwanaume anayetoka naye, jambo ambalo amejaribu kulifanya siri kwa muda mrefu.
 
Miss Tanzania mwaka 2011, Salha Israel.
Salha alifungua kinywa na kubainisha hayo, hivi karibuni alipokuwa kwenye mahojiano na
inayorushwa na mtandao namba moja wa burudani Bongo, 
Akijibu swali la mtangazaji aliyekuwa akifanya naye mahojiano, Luqman Maloto, aliyetaka kujua kuhusu uhusiano wake, Salha alijibu kwa kifupi akisema: “Yeah! Ninaye mchumba.”
: “Anaitwa Moses. Ndiye moyo wangu, maisha yangu, kila kitu kwangu. Nafurahi mwanaume huyu kuja maishani mwangu, maana amekamilisha ndoto zangu. Najivunia kuwa naye kwa kweli.”
 
Hata hivyo, hakutaka kufafanua zaidi kuwa huyo Moses ni nani, anafanya nini na jina lake la pili, kwa maelezo kuwa ni mapema kufanya hivyo.
Huyu hapa anafafanua zaidi: “Hiyo inatosha, ni Moses. Hakuna haja ya mwanaume yeyote kuwaza tena kuhusu mimi. Nafasi imejaa.”
 
“Nawashukuru sana Global TV kwa kunipa nafasi ya kutoa yangu ya moyoni hasa katika kuweka mambo yangu hadharani, najipanga vizuri kufanya mambo makubwa ya kijamii na siyo skendo kama watu wanavyochukulia,” alisema Salha ambaye kwa sasa ametia maguu kwenye tasnia ya filamu za Kibongo