KWA
mara ya kwanza, mzazi mwenza na msanii wa muziki na filamu Bongo,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elias Makala ameibuka na kujinadi hadharani
wilayani Igunga, Tabora. Tukio
hilo lilitokea Februari 14, mwaka huu (Valentine’s Day) ambapo Shilole
aliyekuwa amekwenda kufanya shoo mkoani humo, alishindwa kuzuia hisia
zake baada ya mzazi mwenzake huyo kujitokeza na kujikuta wakioneshana
mahaba mbele za watu.
Pozi
hilo la kimahaba liliwashangaza watu na kuanza kudhani kuwa huenda
wawili hao wakarudisha penzi lao lililokufa miaka mingi iliyopita.
“Mh!
Kweli mtalaka hatongozwi, hebu ona Shilole alivyorembua alipomuona
jamaa yake, pale Makala kumchukua ni kama kumsukuma mlevi,” alisema
shuhuda mmoja.
Baada ya paparazi wetu ‘kuusoma mchezo’ huo, aliamua kumuuliza staa huyo kama penzi lao limerudi upya au laa?
“Hahahahaa!
Kwa kweli unanichekesha kuniuliza kama nimerudisha penzi kwa mzazi
mwenzangu, huyu ni baba wa mwanangu Joyce, itabaki kuwa hivyo. Siwezi
kumtenga na sioni ajabu kupiga naye picha, hakuna kinachoendelea,’’
alisema Shilole.
Licha
ya kufafanua hivyo, usiku wa siku hiyo, Shilole alipokuwa jukwaani
akipagawisha mashabiki kwa shoo kali, alimpandisha jukwaani mzazi
mwenziye huyo hali iliyozua mtafaruku mkubwa kwa mpenzi wa sasa wa
Makala aliyefahamika kwa jina la Maguno.
Baada
ya shoo kuisha, Maguno aliyekuwa na jazba kwa mpenzi wake kupandishwa
jukwaani, alimsaka Shilole kwa udi na uvumba kutaka kumtembezea kichapo
lakini bahati haikuwa yake, hakuweza kumpata hadi msanii huyo aliporejea
jijini Dar siku iliyofuata.
No comments:
Post a Comment