Msanii wa Hip Hop, Roma Mkatoliki amesema kuwa hajawahi kufikiria
kama atakuja kuwa mwanasiasa katika maisha yake, ingawa kuna baadhi ya
viongozi na wadau mbalimbali wamekuwa wakimtaka agombee Ubunge.
Roma amesema kuwa ameshapokea maoni kutoka kwa viongozi mbalimbali
wakimshawishi agombee nafasi ya kisiasa, ila anadai alikataa kwakuwa
anatambua nafasi yake ni ipi katika jamii.
“Toka miaka mitano iliyopita nimekuwa nikiendelea kupokea maoni
mbalimbali kutoka kwa wasanii wenzangu,wananchi wa kawaida na viongozi
wa dini ,viongozi wa serikali, mawaziri wabunge, na kunifuata na
kuniambia nigombee ubunge,” ameiambia Bongo5.
“Sijawai kufikiria kuingia katika siasa kugombea ubunge ama
kujiHusisha na siasa,napenda nisimame kama msanii kwasababu naamini
jukwaa ambalo ninalo ni bora kuliko jukwaa ambalo wanasimama wanasiasa
au kuliko mheshimiwa fulani. Mahubiri yangu ninavyohutubia katika muziki
inawezekana yana nguvu kubwa kuliko hata mtu fulani, kiongozi ama
mbunge wa jimbo fulani. Kwahiyo nafasi ambayo nipo naiona ni nzuri na
sijawahi kufikiria kuingia katika siasa.”
Hata hivyo Roma amesema kuvaa nguo ya chama fulani haimaanishi kwamba yeye ni mwanasiasa.
“Nyimbo yangu mpya kuna mstari unasema ‘Kambarage hakuwa chadema
lakini alivaa ‘track suti’, kwahiyo ni mavazi kama mavazi mengine.
Wakati mwingine tunavaa sana jeans, tunaona ngoja leo nivae kanzu, kesho
nivae suti, kesho kutwa nivae kitenge, hata shule ya msingi zamani
tulikuwa tunanavaa mavazi ya kaki mavazi ambayo hayana tafsiri yoyote.
Kwahiyo mimi navaa chochote kile ambacho kitanivutia hata msanii akitoa
brand nimeipenda ninaweza nikaivaa bila kuangalia tofauti zetu ama
tofauti za watu wengine. Sidhani kama Roma ni mtu ambaye unaweza
ukamtafsiri kwa mavazi. Kwahiyo yale ni mavazi ambayo Roma kama Roma
alivaa lakini Roma hafungamani na chama chochote cha siasa, mimi
nafungamana na sera nzuri, sera ambayo itamkomboa kwa hali kila
Mtanzania.”
Jumatatu ijayo, Roma ataachia wimbo wake mpya, KKK.
No comments:
Post a Comment