Blogger Widgets

March 5, 2014

Mambo Mapya Yaliyoibuka Huko China kwenye Gereza alilowekwa Model Jack Baada ya Kukamatwa kwa Kesi yake Juu ya ,Madawa ya Kulevya

MODO mwenye mvuto Bongo Jacqueline Patrick ‘Jack’, ambaye yuko mahabusu ya Gereza la Qincheng nchini China kwa madai ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini humo, anazidi kuteseka, safari hii akidaiwa kukabiliwa na tatizo kubwa la kiafya.
 
Jacqueline Patrick ‘Jack’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jack anasumbuliwa na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula, hali iliyomfanya apoteze uzito wa kilo kumi huku akikabiliwa na tatizo lingine la kupungua kwa kasi ya mapigo ya moyo. 


KAMA HALI ITAENDELEA
Chanzo kimesema kuwa endapo hali ya kuzorota kwa afya hiyo kutaendelea, Jack anaweza kujikuta katika tatizo kubwa zaidi ambalo linaweza kusumbua kwenye mwenendo mzima wa kesi yake.
“Kusema kweli kuhusu maisha ya mahabusu si mabaya sana kwake, hateswi kwa kupigwa wala hanyimwi chakula, ila hana uhuru binafsi, ni kama amefichwa, naamini matatizo hayo ya kiafya yanatokana na uzito wa kesi yake,” kilisema chanzo hicho. 

MLOLONGO WA MAMBO
Habari zaidi zinadai kwamba kesi ya msingi ya staa huyo kudaiwa kukutwa na madawa ya kulevya itaanza kusikilizwa rasmi Septemba, mwaka huu baada ya mwanasheria wake kukamilisha taratibu zote.

“Ile kesi yake sasa ni Septemba mwaka huu. Si unajua hajawahi kupandishwa kizimbani kuulizwa kama ni kweli alikamatwa na unga au la!” kilisema chanzo hicho.

Jack Patrick akiwa amefunikwa uso baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni nchini China.
WAKILI WAKE ANATOKA HONG KONG
Taarifa zaidi zinasema kuwa wakili wa mrembo huyo anatoka jijini Hong Kong nchini humo ambako ndiko kwenye wanasheria wazuri kwa kiwango cha kesi yake ya unga. 

KUMWONA NI KWA AHADI
Ikazidi kudaiwa kwamba kuna Mtanzania mmoja tu ambaye amekuwa na fursa ya kumuona modo huyo na kabla ya kwenda lazima aombe na kupewa ‘apointimenti’ maalum. 

WALIOMTUMA WAMPIGA CHENGA, WALA ‘BATA’
Tofauti na kwa Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye naye aliwahi kupata msala mkubwa kama huo nchini Afrika Kusini, Julai, mwaka jana ambapo ‘mabosi’ wake walikuwa mstari wa mbele kumhangaikia, Jack anasota mwenyewe.
Habari zinasema kuwa hakuna cheni yoyote kutoka kwa watu ambao wanatafsiriwa kuwa ni waliomtuma kwani wanaosumbuka ni watu wake wa karibu, wakiwemo ndugu zake. 

Juzi, Risasi Mchanganyiko lilizungumza na mtu wa karibu sana na mtuhumiwa huyo ambapo alikiri Jack kuwa na hali ngumu katika kesi yake hiyo huku akisema kwamba watu wanaodaiwa ndiyo mabosi wake wanakula ‘bata’ tu jijini Dar es Salaam. 

“Unajua tatizo la biashara ya unga ni hapo tu! Wewe unayebeba ukinaswa ni juu yako, waliokutuma wao wanachofanya ni kuthibitisha tu kuwa ni kweli umekamatwa maana wapo wanaodaiwa wamekamatwa kumbe si kweli, wanaingia mitini na mzigo,” alisema mtu huyo.  
SABABU ZA MOYO KUSHINDWA KUSUKUMA DAMU
Juzi, gazeti hili lilimtafuta daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (jina lipo) na kumuuliza tatizo la moyo kushindwa kusukuma damu ambapo alisema: 

“Moyo kushindwa kusukuma damu kwa mwendo wa kawaida husababishwa na shinikizo la damu lisilodhibitiwa, mgonjwa kushindwa kudumisha udhibiti wa maji mwilini, chakula au dawa. 

“Sababu nyingine ni upungufu wa damu na utoaji wa kiwango cha juu cha homoni za koromeo ambazo zinaleta maumivu ya ziada kwenye misuli ya moyo, utumiaji mwingi wa vimiminika au ulaji wa chumvi uliopitiliza na utumiaji wa dawa ambazo husababisha uwekaji wa maji mwilini kama vile Hiazolidinedione.” 

KUHUSU KUKOSA HAMU YA KULA
Kwa mujibu wa daktari huyo, tatizo hilo humkumba mtu anapokuwa katika msongo mkubwa wa mawazo kutokana na jambo zito linalomkabili, ambalo halina mlango wa kutokea.
TUKUMBUKE Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau, China akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za heroin tumboni zikiwa na thamani ya jumla ya zaidi ya shilingi milioni 300. 

Awali ilidaiwa kuwa kesi yake ingeanza kusikilizwa mwaka 2016 baada ya yeye kujifunza Kireno (lugha inayotumika Macau) kwa miaka miwili