Blogger Widgets

March 10, 2014

Moja wa Taarifa Iliyowachanganya watu ni hii kuhusu Jack Cliff


Duh! Habari mpya kutoka huko Hong Kong, China zinaeleza kuwa kama atapatikana na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’, modo maarufu Bongo, Jacqueline Fitzpatrick Cliff ‘Jack Patrick’ atatumikia kifungo cha miaka kumi jela.
 
Jack.
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho kilikwenda kumtembelea Jack akiwa nyuma ya nondo baada ya kuruhusiwa kumuona tangu Machi mosi, mwaka huu, mwanamitindo huyo amekata tamaa na hana matumaini ya kutoka jela hivi karibuni.
“Aisee Jack Cliff anatia huruma sana, hana matumaini ya kutoka hivi karibuni na ana maumivu ya kupitiliza,” kilisema chanzo hicho.
 
Jack Patrick akiwa akiwa mikononi mwa polisi nchini China baada ya kukutwa na pipi za heroin tumboni.
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa Jack anasema kuwa kesi yake ni ngumu na endapo atapatikana na hatia, basi atakumbana na kifungo, si chini ya miaka kumi, jambo ambalo limemfanya kudondosha machozi kila kukicha huku akituma salamu nyumbani kwao Bongo.
 
Jack alikamatwa na unga kilo 1.1 huko Macau, Hong Kong mwezi Desemba, mwaka jana ambapo sasa kesi yake itaanza kuunguruma Septemba, mwaka huu.